Sunday, August 31, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMATATU YAKO HAPA

1_4ae62.jpg
2_15e72.jpg

YAMETIMIA CHADEMA--HATIMAYE MBOWE APATA MPINZANI NAFASI YA UENYEKITI,ATINGA MAKAO MAKUU NA WALINZI

KANSA MOHAMED MBARUKU akiwa anasindikizwa na walinzi wake wakati akirudisha form yake ya kugombea uenyekiti katika ofisi za makao makuu ya chama hicho jana jioni.

 Wakati homa na joto la uchaguzi ndani ya chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA likizidi kupanda kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele hatimaye mwanachama mwingine amejitokeza na kuchukua form ya kugombea nafasi ya mwenyekiti wa chama na kufikisha idadi ya watu wawili walioitaka nafasi hiyo huku mmoja akiwa ni mwenyekiti wa sasa na mbunge wa hai mh FREMAN MBOWE.


       KANSA MOHAMED MBARUKU pichani ndiye mwanachadema aliyejitokeza jana jioni kwa ajili ya kupambana na  mwenyekiti wake wa sasa FREMAN MBOWE katika nafasi ya kukiongoza chama hicho katika ngazi ya taifa yani mwenyekiti.

Akizngumza na mtandao huu baada ya kurejesha form hio MBARUKU alisema kuwa lengo la kuitaka nafasi hiyo ni kuhakikisha kuwa chama hicho kinasimama na kuondokana na kashfa mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza hususani za kibaguzi ambazo anasema zinashusha hadhi ya chama hicho.

Saturday, August 30, 2014

MICHEZO--HIVI NDIVYO SIMBA ILIVYOICHAKAZA KMKM USIKU WA LEO.OKWI ASUGUA BENCHI

Beki wa Simba SC, Issa Rashid 'Baba Ubaya' akimtoka mchezaji wa KMKM usiku huu
 IMBA SC imewafunga mabingwa wa Zanzibar, KMKM mabao 5-0 katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

KMKM inayofundishwa na Ally Bushiri ‘Bush’ ambayo Jumatano wiki hii ilifungwa 2-0 na Yanga SC, leo iligeuzwa asusa na Wekundu wa Msimbazi.
Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza mabao 4-0, yaliyotiwa kimiani na Amisi Tambwe mawili, Amri Kiemba na Shaaban Kisiga ‘Malone’ moja kila mmoja.

Wazito; Kutoka kulia Musley Ruwey, Hans Poppe na Salim Abdallah 'Try Again'Amri Kiemba ndiye aliyefungua karamu ya mabao ya Simba SC hii leo, dakika ya tatu ya mchezo baada ya kupewa pasi nzuri na kiungo Mrundi, Pierre Kwizera na kuwatoka wachezaji wawili wa KMKM kabla ya kufumua shuti kali lililogonga mwamba wa ndani wa lango.
Amisi Tambwe akafuatia dakika ya 14 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Salim Amour kufuatia yeye mwenyewe kupiga mkwaju wa penalti, baada ya kiungo, Haroun Chanongo kuangushwa kwenye boksi.
Tambwe tena akafunga bao la tatu dakika ya 23 akimalizia krosi maridadi ya Ramadhani Singano ‘Messi’ kabla ya Kisiga kufunga la nne dakika ya 37, kufuatia kazi nzuri ya Kiemba.

Okwi katikati akiwa na Mosoti kulia na Butoyi kushoto
 Kipindi  ha pili, kocha Mzambia, Patrick Phiri alibadilisha kikosi kizima akimuacha Nahodha Jopseph Owino pekee na dakika ya 60 Elias Maguri akahitimisha karamu ya mabao kwa bao safi la tano.

Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyetangaza juzi kurejea Simba SC kutoka kwa mahasimu, Yanga SC usiku huu alikuwepo, lakini alibaki benchi muda wote wa mchezo.

Amisi Tambwe na Ramadhano Singano 'Messi' kulia wakishangilia usiku huu Amaan

HUYU NDIYE MWANAHABARI ALIYEJITOSA KUGOMBEA UONGOZI CHADEMA

Mmoja wa wachama wa CHADEMA Zanzibar
Bikwao Khamis akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanza
kushoto) anaegombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho kundi la Zanzibar.
Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema
Zanzibar. (Picha zote na Martin Kabemba)
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA Zanzibar Bi
Maryam Ahmed Omar akimkabidhi fomu Salum Mwalim fomu ya kugombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya
Chama hicho kundi la Zanzibar katika hafla fupi iliyofanyika ofisi Kuu za Chadema kisiwani humo.
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar
Jumbe Idrisa akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanza
kushoto) anaegombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho kundi la Zanzibar.
Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyoJumamosiAgosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema
Zanzibar
.
Mbunge wa CAHDEMA viti Maalum wa CHADEMA
Mwanamrisho Abama akimdhamini Mgombe Ujumbe wa Kamati Kuu wa Chama
hicho Salum Mwalim katika ofisi za chama Zanzaibar.
Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisiza Chadema
Zanzibar.
Salum Mwalim anaewania nafasi ya ujumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA
kundi la Zanzibar akitia saini kitabu cha
wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi Kuu za chama hicho Zanzibar kwa lengo la
kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.
……………………………………………..

Friday, August 29, 2014

BREAKING NEWZ--HUZUNI YATANDA MBEYA,AJALI MBAYA TENA,KUMI WAFARIKI HAPO HAPO

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa watu kumi wakiwemo watoto wawili, 
wamefariki dunia papo hapo na wengine 
saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali 
iliyohusisha magari mawili.

Ajali hiyo imehusisha gari ndogo ya abiria 
maarufu daladala lenye namba za usajili T 
237 BFB aina Toyota Hiace na gari kubwa 
aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 
CSV.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo 

wamesema ajali hiyo imetokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea 
Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso 
lililokuwa likiingia barabarani.

Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu 
hayajaweza kupatikana mara moja kutokana 
na kuwa katika hali mbaya huku dereva 
wa Fuso akitokomea  baada ya tukio.

UCHAGUZI CHADEMA MOTO--HUYU NDIYE MGOMBEA WA UMAKAMU WA MWENYEKITI

Na karoli Vinsent
  
     MWANASIASA, wakili wa Mahakama Kuu, Mwanazuoni na mtetezi wa haki za Waislamu nchini, Prof. Abdallah Safari, amejitosa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Taarifa zilizothibitishwa na Prof. Safari mwenyewe zinasema, mwanasiasa huyo mashuhuri nchini anatarajiwa kuchukua fomu wakati wowote kati ya leo na kesho  kuwania moja ya nafasi za juu za uongozi. Ambapo Atawania umakamu mwenyekiti Tanzania Bara.

        Akizungumza na Mtandao mmoja wa Masuala ya kisiasa Nchini muda mfupi uliyopita, Prof. Safari amesema, ameamua kugombea nafasi hiyo ili kutimiza adhima yake ya kuimarisha upinzani na kuhakikisha chama tawala kinaondoka madarakani.

"Nilijiunga na Chadema nikitokea Chama cha Wananchi (CUF). Kule niligombea nafasi ya uenyekiti. Kwa bahati mbaya sana, sikufanikiwa kushinda. Sasa nimejiunga na Chadema na hivyo nataka kile ambacho ningekifanya CUF, nikifanye Chadema," ameeleza.

LIVE TOKA DAR--MANJI ACHARUKA SAKATA LA OKWI,SOMA KAULI ZAKE NZITO LEO

Na Karoli Vinsent
    KUFUATIA mchezaji Emmanuel Okwi kuikacha klabu ya Yanga na kujiunga kwa wapinzania wa Jadi wa timu hiyo, Klabu ya Simba.

     Mwenyekiti wa Klabu Yanga Yusuph Manji ameibuka na kuwataka wanachama pamoja na Mashabiki wa Yanga kuwa wapole katika kipindi hiki,na Badala yake Yanga wamesema wanataka Fidia kutoka kwa Mchezaji huyo pesa za kimarekani dola laki tano, sawa na pesa za Kitanzania zaidi ya milioni 700 kwa kitendo chake cha kuvunja sheria za mpira wa miguu nchini.
            
         Hayo yamesemwa mda huu Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Yanga,Yusuph Manji wakati wa Mkutano na Waandishi  wa Habari kuzungumzia suala nzima la usajili,ambapo Manji amesema klabu hiyo haina ugomvi na Simba kwani wameshirikiana sana kwenye mambo mengi  ila  anashangaa rafu mbaya iliyofanyiwa klabu hiyo,wakati wa kumsajili Emmanuel Okwi.

TIGO NA REACH FOR CHANGE WAZINDUA SHINDANO LA WAJASIRIAMALI JAMII,KILA MSHINDI KUJINYAKULIA DOLA 20,000

Meneja mkuu wa tigo Tanzania DIEGO GUTIEREZ  katikati akizungumza na wanahabari muda huu makao makuu ya tigo wakati akizindua rasmi shindano hilo kulia kwake ni meneja wa REACH FOR CHANGE Tanzania RICHARD GORVETT.
      Kampuni ya mawasiliano ya TIGO Tanzania kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali nchini la REACH  FOR  CHANGE leo wamezindua shindano la  wajasiriamali jamii  liitwalo TIGO DIGITAL CHANGE MAKERS lenye lengo la kuibua mawazo ua kibunifu ambayo yatasaidia kutatua matatizo yanayowakabili watoto na vijana nchini.

Meneja mkuu wa tigo DIEGO GUTIEREZ leo amezindua shindano hilo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo ametoa wito kwa watu kishiriki ili wajiwekee katika nafasi ya kushinda fedha taslim dola 20,000 ambazo kila mshindi atapewa azitumie katika utekelezaji wa mawazo yao ya kibunifu.
 Meneja  huyo alisema kuwa lengo lao ni kupata mawazo ya kibunifu ya kidigitali ambayo yataleta na kutatua matatizo yanayo wakabili watoto kwa kiwango kikubwa huku wakiendelea kuwekeza katika kukuza na kuimarisha huduma zao za mawasiliano katika maeneo yote nchini.

Mawazo yatakayowakilishwa katika shindano hili yanatakiwa kuonyesha uwezo wa kutumia simu kidigital teknologia ya habari na mawasiliano kuleta ufanisi na utekelezaji wa mawazo husika,ambapo amesema kuwa mtu anaweza kutuma mawazo yao kupitia www.tigo.co.tz/digitalchangemakers.

Kwa upande wake meneja wa nchi wa reach for change RICHARD GORVERT amesema kuwa licha ya kupata kitita cha dola 20,000 washindi pia watapewa vifaa vya kuendeleza utekezzaji wa mawazo yao ikiwa ni pamoja na kuapata ushauri kutoka kwa wafanyakazi waandamizi kutoka tigo na reach for change,aidha wataunganishwa na wajariamali wengine ambao tayari wamenufaika na mpango huo.
meneja wa nchi wa reach for change RICHARD GORVERT akizungumza na wanahabari
Mchakato huu wa kuwapata wajasiriamali jamii wa kidigitali  unaenda sambamba na na mkakati wa TIGO  wa kuendeleza maisha ya kidigital nchini.huu ni mwaka wa tatu mfululizo ambapo kampuni ya tigo na reach for change zimekuwa zikishirikiana kuwasaidia wajasiriamali jamii nchini ambapo jumla ya wajasiriamali 6 wamenufaika na mpango huo katika kipindi hiki ambao kwa pamoja na kupitia utekelezaji wa miradi yao wamewasaidia jumla ya watoto zaidi ya 5700 nchini.

Thursday, August 28, 2014

MICHEZO--HIVI NDIVYO EMMANUEL OKWI ALIVYOREJEA SIMBA
Mshambuliaji Mganda Emmanuel Okwi akitambulishwa na mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba Zakaria Hans Pope.
Staili ile ile waliyotumia mahasimu wao Dar es salaam Young Africans kumpata mshambuliaji mganda Emmanuel Arnold Okwi ndiyo ambayo klabu yake ya zamani, wekundu wa Msimbazi Simba SC imeitumia kumrejesha kundini Mganda huyo hii leo
“Tumewaandikia barua TFF kuomba kumtumia mchezaji huyu kwa muda wakati kesi yake na Yanga inaendelea, tumeambatanisha na barua yake ambayo yeye anatuomba kucheza kwetu kulinda kipaji chake,”amesema Poppe.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA AUGOST 29,2014 YAKO HAPA

1_0e849.jpg
2_98cb7.jpg

NI MBOWE TENA CHADEMA

Mwenyekiti wa chama cha demcrasia na maendeleo chadema na mbunge wa jimbo la hai mh FREMAN MBOWE  leo ametangaza rasmi kugombea tena nafasi a uenyekiti wa chama hicho kwa lengo la kuendeleza harakati za chama hicho alizozianzisha.

Hatua hiyo imekuja baada ya wazee wa baraza la wazee chadema na wazee kutoka kigoma  kumwangukia na kumtaka agombee tena huku wakimsifu kuwa amekisaidia sana chama hicho tangu akamate uongozi hivyo ni vyema akaendelea kukiongoza tena chama hicho kwa lengo la kutimiza malengo waliyojiwekea.

Akizungumza katika mkutano wa chama hicho leo jijini dar es salaam MBOWE amesema kuwa amesikia maombi ya wazee hao na yupo tayari kugombea tena nafasi hiyo ya uenyekiti wa chama hicho taifa. huku akiwataka wanachama kuwa na imani na chama chao kwani mapambano bado yanaendelea ya kuwakomboa watanzania.

Aidha MBOWE amesema kuwa wale ambao wanajidanganya kuwa chama hicho kimepungua makali wakae mkao wa kula katika chaguzi zijazo ndio watapata majibu ya mwaswali yao.

Baada ya kukubali ombi ilo wazee hao walimkabidhi mwenyekiti huyo kiasi cha pesa shilingi elfu hamsini kwa ajili ya kuchukua form ya kugombea tena nafasi hiyo ya juu katika chama hicho.VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI WAKUTANA NA KUJADILI USHIRIKI WA MAKUNDI MAALUM KATIKA UONGOZI


Kutoka kushoto ni Dr. Alex Makulilo Mtafiti toka UDSM, Mhe. John Mnyika kutoka CHADEMA , Ndg. Phares Magesa (MNEC) kutoka Chama Cha Mapinduzi na kulia ni mwakilishi kutoka NCCR-Mageuzi !

Tanzania Center for Democracy (TCD) iliwakutanisha viongozi wa vyama vya Siasa wanachama wa TCD ili kupokea taarifa ya Utafiti wa ushiriki wa makundi maalum katika nafasi za uongozi wa nchi, makundi yaliyojadiliwa ni Wanawake, Vijana na Walemavu ... 
Mapendekezo na maazimio ya mkutano huo yanafanyiwa kazi na TCD na baadae yatapelewa kwenye vyama kwa ajili ya kutumia Matokeo ya Utafiti huo ili kuongeza ushiriki wa makundi hayo katika uongozi ndani ya vyama na Taifa kwa ujumla!

BREAKING NEWZZ--MKURUGENZI TBS ATUPWA JELA MIAKA MITATU

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu DSM, imemhukumu kwenda jela miaka 3 aliyekuwa mkurugenzi wa TBS Bwana Charles Ikerege baada ya kukutwa na hatia katika makosa yaliyokuwa yakimkabili, ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.

FUNDISHO KWA WENGINE-MADAKTARI WAWILI WAKAMATWA DAR WAKIMTOA MIMBA MWANAFUNZI,SOMA HADITHI YOTE HAPA

Madaktari wakiwa chini ya ulinzi
 Madaktari wawili, Hamis Chacha na Shengena wa zahanati moja iliyopo Yombo Buza jijini Dar wamejikuta katika wakati mgumu baada ya polisi kuwaibukia na kuwaweka chini ya ulinzi kwa madai ya  kufanya jaribio la kumchoropoa mimba msichana mmoja aliyedaiwa kuwa ni denti wa chuo f’lani cha digrii za juu, Dar.
Madaktari wawili, Hamis Chacha (kushoto) na Shengena wanaotuhumiwa kwa jaribio la utoaji mimba.
 Tukio hilo la aina yake lilijiri Agostii 25, mwaka huu katika zahanati hiyo ambayo jina tunalihifadhi kwa sasa.Awali, wanahabari wakiwa katika pitapita zake walinasa tukio hilo ambapo polisi walikuwa ndani ya zahanati hiyo wakiwaweka chini ya ulinzi madaktari hao.

mtandao huu ulifanikiwa  kuzama ndani ya zahanati hiyo na kuingia kwenye chumba cha kilichodaiwa hutumika katika zoezi hilo.

Vifaa vilivyokusudiwa kutumiwa na madakta hao katika zoezi la utoaji wa mimba.

Wednesday, August 27, 2014

SIKILIZA SAUTI YOTE YA PRESS CONFERENCE ILIYOFANYIKA JUKWAA LA KATIBA LEO

WAZIRI MKUU PINDA AZIDI KUANDAMWA,JUKATA NAO WAMVAANa Karoli Vinsent

       SIKU chache  kupita baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutangaza nia ya kumrithi  Rais Jakaya Kikwete kwenye uchaguzi mkuu mwakani Ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM na kupeleka kuwapa kiwewe wasaka Urais wenzanke ndani ya chama hicho,
        
       Nao Jukwaa la Katiba nchini limeibuka na kusema Kitendo alichokifanya Waziri huyo mkuu kimezorotesha utendaji serikalini kutokana na kauli hiyo kuchochea uhasama kwa watumishi wa Umma.
         
       Kauli hiyo Imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mwenyekiti wa jukwaa la Katiba nchini Hebron Mwakagenda wakati wa mkutano na waandishi wa Habari,ambapo alisema Waziri mkuu huyo alikosea kuzungumza nia yake mapema huku akijua bado ni msimamizi wa Shughuli za serikali.
          

HABARI ILIYOTIKISA JIJI LEO--KATIBA MPYA NI NDOTO KUPATIKANA,JUKATA WAMBEBESHA LAWAMA SITTA.


Kaimu mwenyekiti wa jukwaa la katiba Tanzania HEBRON MWAKAGENDA akizungumza na wanahabri leojijini Dar es salaam
Na Karoli Vinsent  na Exaudi Mtei
         Wakati mchakato wa katiba Tanzania ukiwa ni kama kitendawili kisicho na majibu sahihi kutokana na mchakato huo kuvurugika na kukosa mwelekeo,nao jukwaa la katiba Tanzania  JUKATA wazidi kumtupia lawama zote za kuvurugika bunge hilo   mwenyekiti wa bunge hilo mh SAMWEL SITTA na kudai kuwa ndiye aneyeuvuruga mchakato huo baada ya kugeuza Bunge hilo kama kikao cha Chama cha Mapinduzi CCM.
         
        Akizungumza na wanahabari muda huu jijini Dar es salaam kaimu mwenyekiti wa jukwaa la katiba Tanzania HEBRON MWAKAGENDA amesema kuwa JUKATA wamekuwa wakifwatilia mchakato huu wa bunge ka katiba kwa wiki mbili hizi na kubaini mapungufu makubwa sana ambayo yanatokea jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa mwenyeikiti wa bunge hilo hana nia wala dhamira ya kulipatia taifa katiba mpya ya watanzania.
Wanahabari mbalimbali wakiwa wanamsikiliza kiongozi huyo wakati wa mkutano
        Bw MWAKAGENDA amesema kuwa swala la mahudhurio ya wabunge wanaoshiriki katika kamati mbalimbali za bunge hilo yamekuwa madogo sana na yasiyo ya kuridhisha ikiwa ni pamoja na wabunge wengi kutokuhudhuria katika kamati hizo pamoja na kusaini kulipwa posho za siku jambo ambalo amesema kuwa ni wizi mpya kwa watanzania,

Tuesday, August 26, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMATANO,AUGOST 27,2014 YAKO HAPA

1_28042.jpg
2_d8069.jpg

MICHEZO--DI MARIA ASAINI MAN UNITED

Tumempata! Angel di Maria akikabidhiwa jezi ya Manchester United na kocha wa Louis van Gaal


  HATIMAYE Angel di Maria amekuwa mchezaji wa Manchester United kwa dau la rekodi Uingereza la Pauni Milioni 59.7 usiku huu kutoka Real Madrid.
Winga huyo wa Argentina amesaini Mkataba wa miaka mitano Old Trafford ambao utamfanya apate mshahara wa Pauni Milioni 6.5 kwa mwaka baada ya kodi. 

Hiyo itamfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 awe nyuma ya Nahodha wa United, Wayne Rooney kwa kulipwa mshahara mkubwa. 

SERIKALI YAKABIDHIWA MAGARI NA PIKIPIKI KUTOKA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA UJERUMANI (GLRA) KWA AJILI YA MPANGO WA TAIFA WA KUDHIBITI UGONJWA WA KIFUA KIKUU NA UKOMAMwakilishi Mkazi wa Shirika la Wahisani la Kijerumani linalohudumia Ukoma na Kifua Kikuu (GLRA), Burchard Rwamtoga (wa pili kushoto), akimkabidhi  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid (kulia),moja ya ufunguo wa gari kati ya magari manne na pikipiki 20 vyote vikiwa na thamani ya sh.261,105,615, Dar es Salaam leo, zilizotolewa na shirika hilo kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kupambana na magonjwa hayo nchini. Wanashuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Charles Palanjo na Naibu Waziri, Dk. Steven Kebwe.
Naibu Waziri, Dk. Steven Kebwe (wa pili kulia), na viongozi wengine wa wizara hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Charles Palanjo, Mganga Mkuu wa Serikali Donan Mmbando na Mkurugenzi Msaidizi Afya na Usafi wa Mazingira, Elias Chinamo.
Pikipiki zilizotolewa kwa serikali.
Magari yaliyotolewa kwa Serikali.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid (kulia), akimkabidhi ufunguo wa gari Mratibu wa Huduma za Kifua Kikuu na Ukoma wa Mkoa wa Dk. Deus Leonard katika hafla hiyo.Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid akijaribu kuwasha moja ya magari hayo.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid(kulia), akimkabidhi ufunguo wa gari Mratibu wa Huduma za Kifua Kikuu na Ukoma wa Mkoa wa Kitabibu wa Ilala, Dk.Mbarouk Seif.

HABARI NJEMA KWA WATANZANIA-SASA INAJENGWA RELI TOKA UBUNGO HADI BAGAMOYO,


Na Karoli Vinsent

          KATIKA kukabiliana na tatizo la Msongamano wa Magari Mkoani Dar es Salaam,Serikali imesema iko mbioni kujenga Reli kutoka Ubungo jijini hapa hadi Bagamoyo Mkoani pwani ili kupunguza tatizo hilo kubwa linalowakabili watanzania kwa sasa.
            Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi

 Dkt. Shaaban Mwinjakana  wakati wa mkutano uliowashirikisha wadau wa Masuala ya Reli kutoa nchi tofauti Duniani, Mkutano huo uliofadhiliwa na Serikali ya Japani, ambapo Katibu huyo alisema kwa sasa serikali imejipanga ipasavyo kuhakikisha wanaondoa kabisa Tatizo la Msongamo wa Magari katika Jijini Dar es Salaam,

WALE WACHINA WALIOKAMTWA NA SAMAKI SASA WAMKALIA KOONI MAGUFULI,SASA WANADAI CHAO

Na Kulwa Mzee, kutoka gazeti la Mtanzania

           WACHINA wa ‘samaki wa Magufuli’ walioachiwa huru wanadai meli na samaki zilizokuwamo, ambavyo vyote vina thamani ya Dola za Marekani 3,220,000.

         Mbali na kutakiwa kulipa fedha hizo, pia inatakiwa kulipa Sh trilioni 1.3 ikiwa ni gharama zote, ikiwamo meli, samaki, mawakili na mabaharia wake.

         Hayo yalisemwa  Dar es Salaam jana na Wakili wa Wachina hao, Kapten Ibrahim Bendera na Wakili John Mapinduzi, walipokuwa wakizungumzia hatima ya madai hayo.

   “            Tunadai meli na ikiwezekana na samaki waliokuwamo, thamani ya meli ya Tawaliq 1 kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Uvuvi ni Dola za Marekani milioni 2.5, thamani ya samaki zilizokuwamo ni Dola za Marekani 720,000.
        

VITA YA TANZANIA KWANZA NA UKAWA SASA NI KUCHAFUANA TU,SOMA TUHUMA HIZI TANZANIA KWAZA WALIZOTUPA KWA MBOWE NA SLAA MUDA HUU

Pichani ni mwenyekiti wa kamati ya tanzania kwanza nje ya bunge ndugu AUGUSTINO MATEFU akizungumza na wanahabari muda mfupi uliopita        

        Katika kile kinachoonekana ni kuanza kuchafuana kwa wanasisasa badala ya kutafuta mwafaka wa kuwapatia watanzania katiba mpya Mwenyekiti wa kamati ya Tanzania kwanza nje ya bunge AUGUSTINO MATEFU ameibuka mbele ya wanahabari muda huu jijini Dar es salaam na kutoa tuhuma kali  juu  viongozi wanaoongoza umoja wa katiba Tanzania UKAWA kuwa wana msaada wa kifedha kutoka katika mataifa ya ulaya yanayowasaidia katika kuhakikisha kuwa Mchakato wa katiba haufanikiwi.

PICHA ZA DIMARIA AKIWASILI MAN U USIKU HIZI HAPA


Amenaswa: Di Maria akiwa kiri nyuma kushoto kwenye gari kuelekea viwanja vya mazoezi vya United

KIUNGO Angel di Maria amewasili viwanja vya mazoezi vya Manchester United, Carrington kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wa Pauni 60 kutoka Real Madrid ya Hispania.
Nyota huyo wa Argentina aliyeng'ara kwenye Kombe a Dunia amewasili England huku viongozi wa Old Trafford wakiendelea na mazungumzo na Real Madrid juu ya kukamilisha uhamisho wa dau la rekodi Uingereza.

Di Maria, mwenye umri wa miaka 26, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake usiku huu ambao utamfanya alipwe Pauni 200,000 kwa wiki kwa zaidi ya miaka mitano, mshahara ambao pia utamfanya awe mchezaji wa pili kulipwa zaidi katika klabu hiyo baada ya Nahodha, Wayne Rooney. On the look out: Di Maria peers out of his United car as he arrives for the completion of his trasfer


Uhamisho wote utaigharimu United zaidi ya Pauni Milioni 90 na mchezaji huyo ataingia moja kwa moja katika kikosi kilichojeruhiwa cha Louis van Gaal kwa ajili ya mchezo dhidi ya timu iliyopanda Ligi Kuu, Burnley.