Tuesday, September 30, 2014

TAARIFA KWA WATANZANIA KUHUSU ZITTO KABWE NA CHAMA CHA ACT


ACT-TANZANIA.

ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPERANCY.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Ndugu wanahabari kumekuwa na utaratibu wa habari zinazoupotosha umma wa watanzania kuhusu chama chetu cha ACT-Tanzania.

Katika gazeti la mwanahabari toleo na 117 la tarehe 29/09/2014 katika ukurasa wake wa mbele iliandikwa "MKAKATI WA KUKIPA NGUVU CHAMA CHA KIPYA CHA ZITTO KABWE WAVUJA".

ACT WAZIDI KUIANDAMA CHADEMA,VIONGOZI WENGINE WA CHADEMA LEO WATANGAZA KUHAMIA ACT

Na Karoli Vinsent

     CHAMA kipya cha Siasa cha Alliance for Change and Transparence-Tanzania ACT kiamezidi kukipasua chama cha Demokrsasia na Maendeleo CHADEMA kutokana wimbi la wanachama kukihama chama hicho na kujiunga na ACT.
          
          Wanachama hao kutoka CHADEMA wamejiunga na ACT leo na kupokelewa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar Es Salaam wa chama hicho Hamisi Said Chambuso na kushuhudiwa na Waandishi wa Habari,ambapo Aliyekuwa mwenezi wa baraza la Wanawake la Chadema ,Jimbo la Kawe Batuli Abdalah naye alijiunga na ACT ,
        

TIGO WASHIRIKI KIKAMILIFU KUSAIDIA KUINUA SOMO LA HESABU KWA WANAFUNZI WA TANZANIA

Mkurugenzi wa tigo tanzania DIEGO GUTIEREZ akizungyumza katika hafa iliyoandaliwa na MICROSOFT pamoja na NOKIA kwa kushirikiana na wizara ya mawasiliano sayans na technologia ambapo tigo nao wamechangia kwa kiasi kikubwa katika kutimiza malengo ya huduma hiyo mpya iliyozinduliwa.
  Wanafunzi nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia vifaa vya electronic mfano computer na simu za mkononi  kama njia moja wapo ya kujifunzia na kupata elimu badala ya kutumia kwa nzia zisizofaa.

UPIGAJI KURA WA RASIMU INAYOPENDEKEZWA WAENDELEA LEO BUNGENI MJINI DODOMA.

PICHA 1Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akipiga kura yake kwa ajili ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
PICHA 2Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Hassan Suluhu akipiga kura yake kwa ajili ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
PICHA 3Makamu wa Pili wa Zanzibar ambaye pia Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Seif Ali Idd akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
PICHA 4Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Andrew Chenge akipiga kura yake kwa ajili ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
PICHA 5Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati namba Tano ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Asha-Rose Migiro akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

MICROSOFT LAUNCHES MOBILE MATHEMATICS IN TANZANIA

RIITA VANSK from  Director general of Nokia mathematics project 

 Microsoft, in partnership with the Ministry of Communications, Science, Technology and TigoTanzania,have officially launched an innovative mobile education service called Nokia Mobile Mathematics. This service is now being managed by Microsoft, after the company acquired substantially all of Nokia’s devices and services business.

Nokia Mobile Mathematics is aservice that enables learners across Tanzania toaccess quality mathematics content in an engaging and interactive manner directly from their mobile phones, completely free.
The Guest of honour hon JOHN MNGONDO deputy permenent secretary minister of communication science and Technology speak during the lounching of that services
  

MAMBO SITA AMBAYO BARAZA LA WAZEE LA CHADEMA LIMEITAKA CCM KUWATIMIZIA WAZEE WA TANZANIA

Mwenyekiti wa Baraza la wazee CHADEMA mzee HASHIM JUMA ISSA (katikati) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam kushoto ni makamu wake SUZAN LYIMO na RODRIC LUTEMBEKA katibu wa baraza hilo
Ikiwa kesho tarehe 1,mwezi wa kumi dunia inaadhimisha siku ya wazee  duniani baraza la wazee la chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA limeibuka na mambo sita ambayo wameitaka serikali ya CCM kuwajibu wazee kwani ndio kero za wazee kwa muda mrefu.

Akizungumza na waandiishi wa habari makao makuu ya chama hicho muda huu mwenyekiti wa baraza hilo mzee HASHIMJUMA ISSA ametaja mambo hayo kuwa ni

KIKOSI KIPYA CHA TAIFA STARS KILICHOTAJWA LEO KIPO HAPA


Wachezaji 26 wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa ajili mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kocha Mart Nooij ambaye yuko Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), amesema kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini Oktoba 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Monday, September 29, 2014

PICHA TATU ZA MAANDAMANO YA CHADEMA LEO MANZESE KUPINGA BUNGE LA KATIBA


Wananchi wa manzese ambao ni wanachama wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA leo wamefanya maandamano ya kuendelea kupinga kile wanachokiita ni wizi unaoendelea ndani ya bunge maalum la katiba ikiwa ni mwendelezo wa kutimiza tamko la mkutano mkuu la chama hicho la kufanya maandamano nchi nzima kupinga mchakato huo

TASWIRA TOKA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA LEO

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba, Kapteni John Komba, Bungeni mjini Dodoma Septemba 29, 2014.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Fahmi Dovutwa wakiteta, Bungeni Mjini Dodoma Septemba 29, 2014.

NANI ANAJALI KWA UFISADI HUU WA WAKUBWA

Na Karoli Vinsent

         Tanzania ni nchi ya ajabu kwa mwanadamu makini kuweza kuishi. Ni nchi inayoshangaza sana, ingawa raia wake hawaonyeshi kushangazwa na matukio kadhaa yanayotokea. Naizungumzia Tanzania nchi niliyoishi kwa miongo kadhaa tangu nizaliwe. Baada ya nyimbo nyingi za matatizo, dhiki, wizi, rushwa, tabu, magonjwa na kila aina ya shida ambayo mwanadamu wa kawaida anapitia, jawabu kubwa linapatika kwa swali; nani anajali?

HABARI NZURI TOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA LEO

Na Karoli Vinsent

        MAMLAKA ya Hali hewa nchini(TMA) imezindua Jarida Maalum  lenye kutoa taarifa za matukio ya hali ya hewa kwa mwaka husika ambalo litakuwa likiwapa nafasi wananchi kujua halli ya hewa ya mwaka mzima,

           Uzinduzi wa jarida hilo umefanyika Leo Jijini Dar Es Salam na kushuhudiwa na Waandishi wa Habari pamoja na Wajumbe wa bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA),ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt.Agnes Kijaz alisema Jarida hilo linalengo la ekulezea umma hali ya hewa ilivyokuwa katika kipindi cha mwaka husika kwa ufipi,
     

HUYU NDIYE KIONGOZI WA CHADEMA ALIYEHAMIA CCM KWENYE ZIARA YA KINANA

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiutangazia umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa mikutano Sunga kurejea rasmi kwa Charles Kagonji (mwenye shati la kitenge) kwenye Chama Cha Mapinduzi akitokea Chadema,wengine katika picha hii ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan Mshangama
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiutangazia umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa mikutano Sunga kurejea rasmi kwa Charles Kagonji (mwenye shati la kitenge) kwenye Chama Cha Mapinduzi akitokea Chadema,wengine katika picha hii ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan Mshangama
Mzee Charles Kagonji akiwasalimia wananchi na kutamka rasmi kurejea CCM yeye pamoja na wafuasi wake aliokuwa nao Chadema. Katika mkutano huu wengine waliorudi CCM kutoka Chadema ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo Ismail Semkunde, aliyekuwa Katibu wa Jimbo Mzee Julius Kavurai na aliyekuwa mgombea wa udiwani kwa tiketi ya Chadema Ndugu Ally Gaha.
Mzee Charles Kagonji akiwasalimia wananchi na kutamka rasmi kurejea CCM yeye pamoja na wafuasi wake aliokuwa nao Chadema. Katika mkutano huu wengine waliorudi CCM kutoka Chadema ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo Ismail Semkunde, aliyekuwa Katibu wa Jimbo Mzee Julius Kavurai na aliyekuwa mgombea wa udiwani kwa tiketi ya Chadema Ndugu Ally Gaha.
Wananchi wakinyoosha mikono juu kama ishara ya kumkaribisha CCM Mzee Charles Kagonji.
Wananchi wakinyoosha mikono juu kama ishara ya kumkaribisha CCM Mzee Charles Kagonji.

Saturday, September 27, 2014

NAJUA WAJUA,NATAKA UJUE ZAIDI KUHUSU HILI

Gari hili limetengenezwa nchini ujerumani na kununuliwa na serikali ya Tanzania tarehe 17,desember 1996,Baba wa taifa mwalimu nyerere alitumia gari hili katika shughuli zake mbalimbali za kitaifa hapa nchini pamoja na shughuli zake binafsi hususani katika mikoa ya Dar es salaam na pwanibaada ya kustaafu urais.MERCEDEZ BENZ e300 ndio gari la mwisho kutumiwa na baba wa taifa kipindi cha uhai wake ,gari hili alitumia mara ya mwisho kabisa tarehe 31,augost 1999 kutoka nyumbani kwake msasani kwenda uwanja wa ndege wa kimataifa wa malimu julius nyerere kwa safari ya kwenda london ambapo alikwenda kwa matibabu  ambapo hakurudi tena akiwa hai alifariki huko london,

Gari aina ya AUSTIN MORRIS A40 imetangenezwa nchini  uingereza kati ya mwaka 1940-1950,gari hii ni ya awali kutumiwa na baba wa taifa na rais wa kwanza wa tanzania hayati MWALIMU NYERERE kuanzaia mwaka 1955-1960 katika nshughuli mbalimbali za kuendeleza chama cha TANU,gari hili liliendeshwa na dereva maalum maremu SAID TANU.

Friday, September 26, 2014

HAYA NDIO ALIYOSEMA JAJI WARIOBA JANA NA KUWAACHA WATANZANIA NA MSHANGAO MKUBWA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa na Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalumu la Katiba imeondoa mambo manne muhimu yaliyokuwa kiini cha kupata Katiba ya mageuzi.
Akiyataja mambo hayo muhimu ambayo ni maadili ya viongozi wa umma,  madaraka ya wananchi, mgawanyo wa madaraka na muungano. “Tutakutana mtaani. Tume tutaendelea kutetea rasimu yetu na wao wawaeleze wananchi kwa nini wameondoa maoni yao yaliyokuwa katika Rasimu ya Pili ya Katiba,” aliongeza kwa ufafanuzi Jaji Warioba.

RAIS KIKWETE ATINGA STUDIO ZA CNN -PICHA ZIKO HAPA

President Jakaya Mrisho Kikwete and  CNN's Richard Quest and Maggie Lake when he visited CNN Studios at the Time Warner Building in New York.  This is where Richard Quest produces his world famous "Quest Means Business Programmes".
President Jakaya Mrisho Kikwete and CNN’s Richard Quest and Maggie Lake when he visited CNN Studios at the Time Warner Building in New York. This is where Richard Quest produces his world famous “Quest Means Business Programmes”.
CNN is an American basic cable and satellite television channel that is owned by the Turner Broadcasting System division of Time Warner.
The 24-hour cable news channel was founded in 1980 by American media proprietor Ted Turner. Upon its launch, CNN was the first television channel to provide 24-hour news coverage, and was the first all-news television channel in the United States.
President Jakaya Mrisho Kikwete chats with  Cable News Network (CNN) 's Richard Quest and Maggie Lake when he visited  Time Warner Studios in New York.
President Jakaya Mrisho Kikwete chats with Cable News Network (CNN) ‘s Richard Quest and Maggie Lake when he visited Time Warner Studios in New York.
While the news channel has numerous affiliates, CNN primarily broadcasts from its headquarters at the CNN Center in Atlanta, theTime Warner Center in New York City, and studios in Washington, D.C. and Los Angeles.
CNN is sometimes referred to as CNN/U.S. to distinguish the American channel from its international sister network, CNN International.
 President Jakaya Mrisho Kikwete presents  CNN's Richard Quest when he visited CNN Studios at the Time Warner Building in New York. Right Ms. JulietRugeiyamu Kairuki, the Executive Director of the Tanzania Investment Centre. The Tour was jointly organized by the TIC and CNN as part of an on going partnership to promote Tanzania  as an attractive destination for investment and tourism.  They also discussed  the forthcoming African Journalist of the year Awards Ceremony to be held in Dar es salaam later this year.
President Jakaya Mrisho Kikwete presents CNN’s Richard Quest when he visited CNN Studios at the Time Warner Building in New York. Right Ms. JulietRugeiyamu Kairuki, the Executive Director of the Tanzania Investment Centre. The Tour was jointly organized by the TIC and CNN as part of an on going partnership to promote Tanzania as an attractive destination for investment and tourism.

They also discussed the forthcoming African Journalist of the year Awards Ceremony to be held in Dar es salaam later this year.

FAIDI PICHA NANE ZA MAANDAMANO YA CHADEMA LEO JIMBO LA UBUNGO

Wananchi wa jimbo la UBUNGO  kutoka chama cha CHADEMA leo wameamua kuandamana kwa kile wanachodai kuwa ni kupinga mchakato wa bunge maalum la katiba unaoendelea ambapo hilo ni tekelezo la agizo la mkutano mkuu wa chama hicho

PICHA--WAZIRI MKUU PINDA BUNGENI LEO

PG4A9843[1]Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Peter Serukamba  (kushoto) na Abdulkarim Shah kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 26, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A9894[1]Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba, Abdulkarim Shah (kushoto) na Ayman Jafari kutoka kikundi cha Tulee Yatima Tanzania cha Dar es salaam kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Septemba 26, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A9890[1]Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda , Anna Abdallah (kushoto) na Ave maria Semakafu  wakizungumza kwenye viwanja  vya Bunge Mjini Dodoma Septemba 26, 2014. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)

KUHUSU MAMBO MAKUBWA WALIYOZUNGUMZA UKAWA NA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM USIKOSE HAPA

Mwanasheria wa chama cha democrasia na maendeleo chadema TUNDU LISSU (kushoto) pembeni ni mwenyekiti wa chama hicho mh FREMAN MBOWE pamoja na viongozi wa ukawa walivyokutana na wanahabari leo njijini dar es salaam
Na Karoli Vinsent

LICHA ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta kujinadi kwamba Theluthi 2 ya wajumbe inapatikana wakati wa upigaji kura kuipitisha rasimu  iliyopendekezwa na Bunge hilo, kwa madai wajumbe Bungeni hapo wasiokuwepo watatumia hata njia ya Fax,simu pamoja na “Internet” mtandao  kupiga kura,
           
Nao Viongozi Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA umemjia juu Rais Jakaya Kikwete kwa kitendo chake cha Kumwacha mwenyekiti wa Bunge hilo Samwel Sitta kwa kuendelea kufanya hujuma kwa watanzania kwenye mchakato wa katiba,
         
  Kwani Duniani kote hakuna kura yeyote inayopigwa kwa njia ya simu wala Internet na anavyofanya hivyo samweli sitta ni kutaka kufanya mambo pasipo kisheria,
           
Hayo yamesemwa mda huu Jijini Dar es Salaam na Viongozi wa  vyama vikuu vya upinzani nchini wanaounda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba alimshangaa Rais Jakaya Kikwete kwa kuyakimbia matatizo nchi na kwenda nje ya nchi na kushindwa kuliokoa taifa katika hujuma  anayofanya Samwel sitta.
        
“Rais Kikwete amekuwa mtu wa kwenda Marekani kila wakati yanapotokea Matatizo,na leo anamwacha Samwel Sitta anafanya mambo ya ajabu, ambayo duniani hayajawai kutokea kura kwa njia ya simu,harafu Rais Kikwete anashindwa kukemea uragai huu,hivi huyo ni kiongozi gani”Alihoji Profesa Lipumba
           


Profesa Lipumba ambaye ni Gwiji la masuala Uchumi kimataifa alizidi kuzungumza kwa Uchungu ambapo alimshangaa Rais Jakaya Kikwete kuonyesha ugeugeu kwa watanzania kwani wakati wa Mkutano kati yake na Vyama vya kisiasa nchini vilivyo chini ya Kituo cha Demokrasia nchini ( TCD).
          Katika mkutano huo Rais Kikwete alikubali wazi kwamba bunge Maalum la sasa aliwezi kuleta katiba cha kushangaza leo  ameshindwa hata kuingilia kati utoto unaofanywa na Samwel Sitta kwa Watanzania.

Thursday, September 25, 2014

WANAFUNZI WA TAMBAZA WAPEWA SOMO NA TAASISI YA WAANDISI NCHINI

Na Karoli Vinsent

       KATIKA kuonyesha imedhamiria  kuhakikisha wanapatikana Waandisi bora nchini,Taasisi  ya Waandisi Nchini(Istitution of Engineer Tanzania IET) imewataka wanafunzi  kuacha kusomea masomo ya sanaa peke yake badala yake wajikite zaidi kwenye masomo ya sayansi ili kulisaidia Taifa liweze kupata waandisi wenye sifa,

TAIFA STARS, BENIN KUCHEZA DAR OKTOBA 12

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inashuka uwanjani Oktoba 12 mwaka huu kuikabili Benin katika mechi ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Programu ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa ajili ya mechi hiyo itatangazwa baadaye na Kocha Mkuu Mart Nooij.

KAULI YA BAWACHA KUHUSU RASIMU ILIYOPENDEKEZWA JANA

HALIMA MDEE mwenyekiti wa BAWACHA akizungumza nna wanahabari Jijini  Dar es salaam.
            Baraza la wanawake wa chama cha democrasia na maendeleo chadema BAWACHA wamekuwa wa kwanza kuipinga rasimu ya tatu iliyowasilishwa bungeni jana na kutangaza kuandamana hadi ikuliu ya jiji la dar es salaam kupeleka kilio chao kwa kile walichoitwa kushindwa kuwapa wanawake nafasi stahiki katika rasimu hiyo

           Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam mwenyekiti wa baraza hilo BAWACHA ambaye pia ni mbunge wa kawe HALIMA MDEE amesema kuwa kuwapa wanawake nafasi za uongozi za hamsini kwa hamsini kama rasimu hiyo ilivyoelekeza bado sio kipaumbele cha wanawake wa Tanzania ila kinachofanyika ni kuendelea kuwalaghai wanawake wa Tanzania.

            Aidha amesema kuwa rasimu hiyo bado haimjali mtanzania kwani kuna mambo mengi ambayo yameondolewa yalikuwepo kwenye rasimu ya WARIOBA.

            Wanawake hao wametangaza kufanya maandamano wiki moja ijayo ambayo amekataa kutaja siku rasmi kwa kile alichokisema kuwa bado wanafanya maandalizi ambapo yatakuwa  ya amani ambapo amewataka polisi kuwalinda kwani maandamano hayo yatakuwa ya amani na utulivu mkubwa yakiwa na lengo la kupeleka ujumbe kwa watanzania wote juu ya mchakato huo wa katiba.

HOT NEWZZ--CHUO CHA IMTU CHAFUNGIWA

Na karoli Vinsent


           TUME  ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) Imekifungia kwa mda,Chuo kikuu cha tiba na Sayansi IMTU  kutofanya udahili kwa Wanafunzi wapya wa Mwaka wa Masomo 2014-2015,kutokana na chuo hicho kukiuka sheria inayosimamia Vyuo Vikuu nchini.
        
             Uamuzi huo wa kikifungia Chuo hicho Umetangazwa mda huu Jijini Dar Es Salaam na Kaimu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU)  Profesa Magishi N Mgasa wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari ambapo alisema maamuzi hayo yamefikiwa baada kikao cha Dharura kilichoitishwa na (TCU) wiki iliyopita na kujadili taarifa ya timu iliyotathimini chuo hicho,
        
          Ambapo kikao hicho kikabaini mapungufu makubwa katika chuo cha IMTU yakiwemo matatizo ya uongozi,kukosa wahadhiri wakutosha na wenye sifa,kutokuwepo na Vifaa pamoja na kudahili wanafunzi bila hata kuwa na taratibu zilizowekwa na tume,
    
          Profesa Mgasa alisema kwa kufanya hivyo chuo cha IMTU imekiuka sheria ya namba 5(1),sura ya 346 ya sheria za Tanzania ambayo inakitaka chuo Kikuu chochote kufuata taratibu zilizowekwa na tume,
     
         Vilevile Profesa Mgasa alizidi kusema baada ya Tume kubaini makosa hayo,ndipo wamefikia maamuzi ya kukifungia chuo cha IMTU kufanya udahili kwa wanafunzi wapya wa Mwaka 2014-2015,mpaka pale itakakaporekebisha mapungufu yaliyotajwa na Tcu,
       
          Pia tume imetoa notisi ya miezi 3 kwa chuo cha IMTU,kuanzia tarehe 16 mwezi huu kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza na endapo chuo hicho kikikaidi basi TCU haitosita  kuwachukulia hatua kali ikewemo hata kukifungia kabisa.
        
          Aidha Profesa Mgasa aliwataka wanafunzi nchini wasijiunge na chuo Kikuu chochote  bila ya kufuata maelekezo kutoka Tume ya vyuo Vikuu nchini (TCU).

Wednesday, September 24, 2014

HIKI NDICHO ALICHOKIFANYA BAKHRESA KWA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO TANZANIA LEO

Meneja Mkuu wa SSB, Sheikh Said Muhammad (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya Sh. milioni 10 kwa Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto (kulia). Wanaoshuhudia ni viongozi wengine wa TASWA kutoka kushoto Shijja Richard (Mweka Hazina), Amir Mhando (Katibu Mkuu) na Egbert Mkoko (Makamu Mwenyekiti).

KAMPUNI ya Said Salim Bakhresa Group Limited, leo imetoa kiasi cha Sh. Milioni 10 kwa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kwa ajili ya tuzo za Wanamichezo Bora nchini, zilizopangwa kufanyika Desemba 12, mwaka huu.


  Akikabidhi fedha hizo, Meneja Mkuu wa SSB Limited, Sheikh Said Muhammad Said katika ukumbi wa City Sports Lounge, Mtaa wa Samora, Dar es Salaam, amesema kwamba wanatoa mchango huo ili kuwezesha zoezi hilo lifanikiwe.
“Kwanza nasema naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa niaba ya kampuni kwa TASWA kutufuata kutuomba tuchangie tuzo hizi. Sisi tupo mstari wa mbele katika kuunga mkono harakati zote za kimaendelea katika sekta ya michezo nchini,”amesema.Sheikh Said amesema kwamba SSB inajivunia kuwa sehemu ya shughuli hiyo na inawatakia kila la heri TASWA ili wafanikishe mchakato huo.

SIRI IMEFICHUKA--MAGAZETI YA NIPASHE,TANZANIA DAIMA NA MAWIO HATARINI KUFUNGIWA,SOMA CHANZO HAPA

Na karoli Vinsent

     SERIKALI ya Tanzania  imezidi kuuzika uhuru wa Habari nchini kutokana na sasa kuanza kuvifungia vyombo vya Habari hususani Magazeti,baada ya hivi sasa serikali  kujiweka tayari kuyafungia magazeti ya Nipashe,Tanzania Daima pamoja Mawio,Mtandao huu unaripoti
        
       Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu umezipata zinasema serikali imejipanga kuyafungia magazeti hayo kutokana na habari wanazoziandika ambazo serikali inaziita ni za uchochezi,
       
         Kwa mujibu wa Vyanzo mbalimbali zinasema serikali imekasirishwa na Habari wanazoziandika magazeti hayo kuhusu mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba  ambazo wanadai habari hizo zinaleta mgongano kwa wananchi,
       
        Mpashaji huyo wa Habari aliuambia mtandao huu kwamba kwasasa serikali imejipanga kuhakisha inayafungia magazeti hayo.
       

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA MWAKA LA WAKAGUZI WA HESABU ZA NDANI JIJINI ARUSHA LEO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua Kongamano la mwaka la siku tatu la Wakaguzi wa Hesabu za Ndani, linaloendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha. Kongamano hilo limefunguliwa leo Septemba 24, 2014. Picha na OMR

 Baadhi ya washiriki waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia katika ukumbi wa AICC jijini Arusha leo Septemba 24, 2014.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia burudani ya ngoma ya asili wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa AICC jijini Arusha leo Septemba 24, 2014 kwa ajili ya kufungua Kongamano la mwaka la siku tatu la Wakaguzi wa Hesabu za Ndani. Picha na OMR

Tuesday, September 23, 2014

BREAKING NEWZ--YAMETIMIA BUNGE LA KATIBAMH. CHENGE AWASILISHA RASIMU YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA KWA MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA.

Hayawi hayawi yamekuwa sasa. Ile KATIBA INAYOPENDEKEZWA yatoka rasimi leo.
Imekabidhiwa kwa Mwenyekiti na kesho (24/09/2014) itawsilishwa rasmi kwenye Bunge zima la Katiba.
Pichani Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba Mhe. Andrew Chenge akimkabidhi Mwenyekiti wa Bunge hilo Mhe. Samuel Sitta Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi cha Bunge hilo leo (23/09/2014).
Kamati ya Uandishi imemaliza kazi ya kuandaa Rasimu hiyo na inatarajiwa kusomwa Bungeni kesho.


TAARIFA KWA UMMA KUKANUSHA UVUMI WA KUAJIRI VIJANA 500 NA KUWAPATIA MASOMO YA MAFUTA NA GESI-TPDC

SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA
Tanzania-Petroleum-Development-Corporation-TPDC
Kuna taarifa zimeendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na maelezo kuwa: ” Serikali kupitia Shirika la Elimu Tanzania, TPDC kwa ushirikiano na kampuni za oil and gas, wanatarajia kuajiri vijana wapatao 500 katika sekta hii mpya Tanzania kuanzia mwezi Januari na Machi 2015, hivyo 
wameandaa crush program itakayoanza 6 Oktoba 2014. Walengwa ni vijana wenye elimu ya form 4 na form 6 ambao watasoma kwa miezi 6 na kupelekwa kwenye ajira  moja kwa moja baada ya kuhitimu!..kwa wale wenye elimu kuanzia diploma watasoma kwa miezi 3, kozi ya oil and gas management!…Ada kwa kundi la kwanza ni tshs 1,150,000 na kundi la pili ni Tsh 550,000. Kwa yeyote mwenye kuhitaji fursa hii akachukue fomu Shirika la Elimu Tanzania, application form ni Tsh 20,000 na deadline ni tarehe 30 Septemba 2014″.
TPDC inapenda kuwaeleza Watanzania kuwa habari hizo si za kweli na kwamba TPDC haijafanya makubaliano yoyote na Shirika la Elimu kuhusu suala hilo. TPDC inawaasa Watanzania kuchukua tahadhari ya matangazo ya aina hiyo na inapotokea, tafadhali wasiliana nasi kwa namba za simu zilizooneshwa hapo nchini.
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO,
SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA
                  BWMPensions Towers, TowerA,
                    Junctionof Azikiwe /JamhuriStreets
                  P. O. Box2774,
                  Tel: +255 22 2200103/4
           Dar-es-Salaam, Tanzania

PRESIDENT KIKWETE IN DIFFERENT ACTIVITIES IN NEW YORK

 President Jakaya Mrisho Kikwete greets Senator Chris Coons of Delaware who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
  President Jakaya Mrisho Kikwete invites  Senator Chris Coons of Delaware and Chairman of  Perdue Farms Mr Jim Perdue who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
 President Jakaya Mrisho Kikwete in talks with  Senator Chris Coons of Delaware and Chairman of  Perdue Farms Mr Jim Perdue and their delegation who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 

LHRC-BADO WANANCHI HAWANA UELEWA WOWOTE WA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi HELEN KIJO BISIMBA akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam
             Ikiwa mchakato wa katiba mpya ukiendelea kwa bunge maalum la katiba kufikia hatua ya kuipigia kura rasimu iliyopendekezwa na kisha kuletwa kwa wananchi,imeelezwa kuwa bado watanzania wengi hususani wale ambao wapo pembezoni mwa nchi hawana uelewa wowote juu ya mchakato huo na hatua unaopitia.
         
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC  Bi HELEN KIJO BISIMBA wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu awamu ya pili ya kampeni ya kusambaza uelewa wa rasimu ya pili (KAMPENI GOGOTA),kampeni iliyofanyika katika mikoa ishirini ya tanzania.
        
      Bi HELEN amesema kuwa katika mikoa mingi waliopita moja ya changamoto kubwa waliyokutana nayo ni wananchi wengi kukosa uelewa kabisa wa katiba mpya jambo ambali amesema kuwa linazua hofu kubwa  kama wakipelekewa rasimu iliyopendekezwa kama watakuwa tayari kuipitisha hata kama  hawajaelewa na si ile iliyotokana na tume ya mabadiliko ya katiba tanzania.

Monday, September 22, 2014

SERIKALI YAWATEMA WAANDISHI WALIOPIGWA,YASEMA HAKUNA MWANDISHI ALIYEPIGWA WOTE NI WANACHAMA WA CHADEMA

Na Karoli Vinsent

        HUKU wadau mbalimbali wa Habari wakiwa wanalaani Vikali kitendo cha Jeshi la polisi kuwapiga wanahabari wakati wakiwa kazini,tukio hilo lilitokea Mwishoni mwa wiki iliyopita Makao makuu ya Jeshi la polisi nchini ambapo mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe alipofikishwa  polisi,
          
           Katika hali ya kushangaza Serikali imesema haina taarifa juu ya kupigwa kwa mwandishi,bali imesema inafahamu tu wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ndio waliokwenda makao makuu ya Jeshi la Polisi,na hawafamu kwamba kunawanahabari waliopigwa,