Tuesday, January 13, 2015

DIAMOND NA ALIKIBA JUKWAA MOJA DAR ES SALAAM,NI TAMASHA LA TIGO MUSIC,NI HUDUMA MPYA YA TIGO KUWANUFAISHA WASANII

Msanii wa music wa kizazi pipya diamond akizungumza na wanahabari juu ya huduma hiyo na jinsi alivyoipokea
Kampuni ya  simu ya TIGO TANZANIA leo imetangaza uzinduzi wa muziki wa tigo ujulikanao kama TIGO MUSIC kwa kushikiana na DEEZER ambayo ni huduma ya kimataifa inayorusha music itakayowapa watanzania music usiokuwa na kikomo.
Mwana FA naye ni mmoja kati ya wale ambao watakuwa katika show hiyo ya uzinduzi pale LEADERS CLUB 

Akizundua huduma hii mpya meneja wa chapa wa TIGO WILLIAM MPINGA amesema kuwa kuanzia January 24,wateja wa tigo wenye vifurushi vya malipo ya kabla ya internent wana uwezo wa kupata nyimbo million 36 za wasanii wa kitanzania na Africa kwa ujumla katika simu zao za mikononi na za smartphone.

Amesema kuwa vile vile tigo itatafuta miziki mipya ya kusisimua ya wasanii wa ndani kupitia ushirikiano mpya wa kampuni ya Africa music rights ambayo inawezesha kutafuta na kusimamia haki za music katika bara la Africa .
Ali Kiba atakuwepo
 Huduma hiyo itazinduliwa rasmi mnamo January 24 mwaka huu katika viwanja vya leaders ambapo kutafanyika hafla ya uzinduzi ambapo wananchi watapata burudani ya kutosha kutoka kwa wasanii maarufu na mahiri kutoka Tanzania kama diamond,alikiba,profesa j,vanesa mdee,ben paul,isha mashauz,malaika band,yamoto band,msondo,na wengine kibao kutoka Tanzania ambapo kiingilio kitakuwa ni bure Tamasha ambalo limepewa jina la KIBOKO YAO
Weusi nao walizunguma na wanahabari juu ya jinsi walivyojiandaa na show hiyo 

Aidha amesema kuwa mabali na kuwapa wateja nafasi ya kupata music kupitia huduma hiyo pia wasanii wa Tanzania itakuwa ni nafasi kwao ya kujiongeea kipato kutokana na nyimbo zao ambazo zitakuwa zimesikilizwa kupitia huduma hii ambapo tigo itawapa wasanii hao mafunzo jinsi ya kutumia na kunufaika na huduma hii.
Meneja wa chapa wa TIGO WILLIAM MPINGA akizngumza na wanahabari juu ya huduma hiyo



Kuanzishwa kwa huduma hiyo ya TIGO MUSIC nchini Tanzania kumetokana na mafanikio ya uzinduzi wake nchini Ghana mwaka 2014 na America ya kusini mwaka 2012,tangu kuanzishwa kwake imekuwa ni sehemu muhimu kwa maisha ya kidigital ya watu ya kila siku nah ii inaendana na matukio ya music ya ana kwa ana yaliyowahi kufanywa na wanamusic mashuhuri duniani pamoja na yale yaliyorekodiwa ndani ya studio
PICHA ZAIDI ZIPO CHINI------------








No comments: