Friday, January 9, 2015

HABARI KUBWA LEO,WAISLAM WATANGAZA KUIPIGIA KURA YA HAPANA KATIBA PENDEKEZWA

 Kaimu Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, SHEKH RAJAB KATIMBA akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam. 
NA KAROLI VINSENT
               
JUMUIYA na Taasisi za Kiislam Nchini imesema itawahamasishwa Waumini wa Kiislam popote walipo nchini kuipigia kura ya Hapana katiba iliyopendekezwa na Bunge maalum  la Katiba, pamoja na kuukataa Mswaada wa Marekebisho ya sheria mbalimbali wa namba 2 wa mwaka 2014 unaotarajiwa kuwasilishwa kwenye Bunge lijalo  kutokana na Serikali kuwadanganya waislam nchini.
          
     Kutokana na kitendo chake Serikali kupuuza matakwa yao wanaodai uwepo wa Mahakama ya Kadhi ambao wanasema ilikuwepo kwenye makubaliano kati ya Serikali na Waislam nchini juu ya uwepo wa Mahakama hiyo.
Wanahabari mbalimbali wakisikiliza kwa makini
           Hayo yamesemwa Leo Jijini Dar Es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, Rajabu Katimba wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo alisema waislam wamechoka na ubabaishaji  unaofanywa na serikali ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kulitekeleza Azimio la uundwaji wa Mahakama ya Kadhi nchini.

      
 “Kwani hata mswaada wa marekebisho ya kisheria mbalimbali unaowasilishwa na serikali hautakuwa na tija kwa waislam nchini na umekuwa na propaganda nyingi  za unzishwaji wa mahakama ya kadhi lakini hauna utekerezaji na ndio sababu tunasema hakuna nia ya dhati kati ya serikali ya CCM na Waislam”
       
“Nchini kwani wametudanganya kwenye Ilani yao ya Mwaka 2005 ilituhaidi kuanzisha mahakama ya kadhi lakini kwa ghilba nyingi CCM haikutekeleza ahadi hiyo baada ya kuingia madarakani kwa hoja kuwa hili ni  Jambo la Kikatiba”alisema katimba
       SHEKHE  Katimba alizidi kusema kwa Uchungu kwamba 

“hata wakati wa Bunge la katiba  lilokuwa limeundwa na wajumbe wengi wa CCM hawakuona umuhimu  wa kutimzi ahadi yao ya kuweka Mahakama ya Kadhi katika katiba pendekezwa na kwani wajumbe wengi wa CCM walishangilia Jambo hili ili hali wanajua Dhahiri kuwa Waislamu hawakufurahishwa na uamuzi wao na pia walikiuka ilani yao na ahadi kwa Waislam”
        
Aidha,Shekhe Katimba alisema hata mswaada ambao wanaukataa wa merekebisho ya Sheria wa namba 2 wa mwaka 2014 unakasoro nyingi ambazo wanasema hauna tija kwa waislam katika kipengere cha Mahakama ya Kadhi-
     Ikiwemo Mswaada umempa mamlaka “MUFTI”kuteua makadhi na kuengeneza kanuzi za Uendeshaji wa mahakama ya Kadhi ili hali sio chombo cha Sheria,na pia  Mswaada huo umempa Mufti-
         
Mamlaka ya kutenganisha kanuni za uendeshaji wa mahakama za kadhi ambalo wanasema ni jambo la ajabu kwani ofisi ambayo haiundwi na sheria na mamlaka ya kuengeneza kanuni za chombo.
        
Shekhe Katimba alisema hata Mswaada wa kuikataa ,mahakama ya kadhi ijiendeshe yenyewe badala ya kuendeshwa na Serikali ni Jambo ambalo haijawahi kutokea Sehemu yeyote duniani Chombo, kama mahakama kujiendesha yenyewe.
      
Hata Hivyo Shekhe Katimba aliwataka waislam kwa Ujumla kutoipigia kura ya Ndio wakati wa kupigia kura katiba iliyopendekwa na Bunge mwezi March mwaka huu kwakuwa katiba hiyo haina nia nzuri kwa Waislam nchini





No comments: