Vodacom yazindua promosheni ya shilingi bilioni 30 ----300m/- kushindaniwa kila siku!

Balozi wa promosheni ya JayMilions Hilary Daud”Zembwela”(kushoto)akionesha bango linaloelezea jinsi ya mteja kujua kama ameshinda katika Promosheni hiyo iliyozinduliwa na Vodacom Tanzania  leo itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia zawadi mbalimbali zenye thamani ya Shilingi Bilioni 30/- Ili kujua kama umeshinda mteja anatakiwa kutuma SMS moja tu kila siku yenye neno “JAY” kwenda namba 15544.Wengine kutoka kulia Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo Kelvin Twissa.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(katikati)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa Promosheni mpya inayojulikana kama JayMillions itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia zawadi mbalimbali zenye thamani ya Shilingi Bilioni 30/- Ili kujua kama umeshinda mteja anatakiwa kutuma SMS moja tu yenye neno “JAY” kwenda namba 15544 kila siku.Kushoto ni Balozi wa promosheni hiyo Hilary Daud”Zembwela” na kulia ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.

 Vodacom imezindua promosheni kubwa kuliko zote katika historia ya michezo ya bahati nasibu nchini Tanzania ambapo wateja watajishindia pesa taslimu Sh. bilioni 30/- katika zawadi ndani ya kipindi cha siku 100.

Akizungumza na waandishi wa habari jjijini leo ,Mtendaji   Mkuu  wa Vodacom Tanzania Rene Meza amesema promosheni hii inajulikana kama JayMillions na inawahusisha wateja wote wa Vodacom na ni ya kwanza ya aina yake kwani, “kiasi kikubwa cha fedha kitatolewa kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki.”

Vodacom itatoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/-, washindi kumi wa Sh. 10m/- na washindi mia moja wa Sh. 1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/- kila siku.

Meza ameongeza kuwa hii inadhihirisha dhamira ya kampuni ambayo mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wake pia ina dhamira ya kubadilisha maisha ya wateja kuwa murua zaidi “ambao wamekuwa wakiendelea kujiunga na familia ya Vodacom kila siku.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa amesema ili kushiriki katika promosheni hii, mteja yeyote wa Vodacom, aliyeko popote nchini anahitaji kutuma SMS moja tu yenye neno “JAY” kwenda namba 15544 kila siku ili kujua kama ameshinda au la. Mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu.

“”Tofauti na promosheni zilizopita, JayMillions ni rahisi sana kushiriki. Tuma ujumbe mfupi mmoja tu na mara moja tu kila siku. Hakuna maswali mengi, wala chemsha bongo na hivyo kufanya hii kuwa promosheni inayotoa nafasi kwa wateja wengi kuibuka washindi. Cha muhimu ni kuhakikisha kila siku unatuma ujumbe mfupi,” alieleza Twissa.

Alisema kila siku namba zilizoshinda zitapatikana kupitia mfumo mahsusi wa promosheni hii. “Ili kujua kama namba ya mteja imechaguliwa, tunapenda kukusisitizia mteja wetu kutuma ujumbe mfupi wa “JAY” kila siku kwenda 15544 ili wasipoteze bahati zao iwapo namba zao zitakuwa zimechaguliwa. Bila kufanya hivyo, wanaweza kupoteza mamilioni kwani hawatoweza kujua kama namba zao zilichaguliwa kama washindi ambapo zinachaguliwa kila siku,” alisisitiza Twissa.

Mwisho

Kuhusu Vodacom Tanzania
Kampuni ya Vodacom Tanzania ni kampuni inayoongozwa kwa kuwa na mtandao mkubwa na huduma za mawasiliano nchini. Ilianza kutoa huduma nchini mnamo mwaka 2000, ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) ya Afrika ya Kusini ambayo pia ni kampuni tanzu ya  Vodafone Group UK.Vodacom Tanzania Limited hisa zake zinamilikiwa kwa pamoja na makampuni ya Vodacom Group (Pty) na Mirambo Ltd.

Vodacom inaongoza katika soko na kutoa huduma bora za mawasiliano nchini, na imekuwa mstari wa mbele kubuni huduma bora za mawasiliano za kuwarahisishia wateje wake maisha. Moja ya huduma inayotolewa na Vodacom ambayo imeleta mabadiliko makubwa nchini ni M-PESA ambayo hadi sasa inatumiwa na wateja zaidi ya milioni 5.2. Zaidi ya taasisi 200 nchini zinapokea malipo kupitia M-PESA. Huduma hii ni suluhisho katika kufanya malipo kwa kuwa utumiaji wake hauhitaji  mpaka uwe na akaunti ya benki. Hapo ndipo umuhimu wa huduma hii unaonekana kwakuwa idadi kubwa ya watanzania hawana sifa za kufungua akaunti za benki na idadi ya wenye akaunti ni wachache. Kwa kupitia M-PESA, mteja wa Vodacom anaweza kuweka akiba inayofikia milioni 5 katika simu yake, anaweza kutuma, kupokea fedha na kutoa fedha kutoka kwa mtandao wa mawakala wanaotoa huduma hiyo ambao wameenea nchini kote. Mteja pia anaweza  kuangalia salio la akaunti yake ya benki akiwa nyumbani.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.