Tuesday, January 13, 2015

Wadau wa Social Media Network Citizens wachangia madawati kwa shule ya Msingi Mjimwema

 Mbunge wa Kigamboni (kulia) akikabidhi MOJA ya dawati kwa Mwalimu Mkuu (Kushoto) huku wakishuhudia na Bw Irinei Kiria (Mbunifu wa harambee hii), Bi Germana Ibreck (Mtunza fedha), Dkt Mwele Malecela na Afisa Elimu toka Manispaa ya Temeke.
 Siku ya tarehe 11.01.02 wadau wa "Social Media Network Citizens", ambao ni watumiaji wa  mtandao wa kijamii wa Twitter walifanya awamu ya pili ya zoezi la kukabidhi madawati 241 kwa shule ya msingi ya Mjimwema iliyopo kwenye kata ya Mjimwema, Jimbo la Kigamboni.
Katika awamu ya kwanza, wadau hawa walikabidhi madawati 45. Jumla ya Tsh 30.5 millioni zimechangwa na wadau hawa na zimetumika kutengeneza madawati 286 yaliyotolewa hadi hivi sasa.

Mchango huu wa madawati umewezesha kutatua tatizo la madawati kwenye shule hii kwa asilimia 80% na kuwezesha wanafunzi 858 ambao ni asilimia 75% ya wanafunzi wote kukaa kwenye dawati.

Mgeni Rasmi kwenye makabidhiano haya alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dkt Faustine Ndugulile.
Mgeni Rasmi, Mbunge wa Kigamboni, akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Social Media Network Citizens na walimu.
 Mwisho, shule hii bado inahitaji madawati 70 ili watoto wote waweze kuwa na dawati. Vile vile Ofisi za walimu zina upungufu wa samani. Wadau wameanza raundi ya tatu ya michango kwa ajili ya kumaliza tatizo la madawati kwenye shule hii.
Wadau wanaotaka kuchangia wanakaribishwa kuwasiliana na waratibu (@AnnieTanzania na @IrineiKiria) kupitia mtandao wa Twitter.
Mtunza fedha wa Social Media Network Citizens Bi Germana Ibreck akiwa na wanafunzi wa shule ya Mjimwema.

No comments: