Wednesday, February 18, 2015

BAADA YA LIPUMBA,HUYU NAYE AMETANGAZA KUGOMBEA URAIS UKAWA

Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dk Emmanuel Makaidi.
Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dk Emmanuel Makaidi.
Vuguvugu la Urais ndani ya umoja wa Katiba ya Wanachi UKAWA linazidi kushika kasi kufuatia Mwenyekiti wa CUF prof. Ibrahim Lipumba kufungua pazia la kupelekwa jina lake UKAWA ambapo  Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dk Emmanuel Makaidi naye  ametuliwa kuingia katika kinyang’anyiro cha kugombea urais  ndani UKAWA.

Mwenyekiti  wa Chama cha NLD, Dk Emmanuel Makaidi amesema tayari chama chake kimeshapendekeza jina lake kuwa miongoni mwa vigogo watakaoshindanishwa kwenye kinyang’anyiro hicho ili lipatikane jina moja litakaloiwakilisha UKAWA kupambana na chama tawala cha Mapinduzi.
Aidha, makubaliano ya umoja huo yanaelekeza vyama kupendekeza jina moja litakalowakilishwa katika Kamati ya Wataalamu ya Ukawa kabla ya kushindanishwa na majina mengine.

Kwa upande wa  Vyama vya NCCR Mageuzi na Chadema bado havijaonyesha mwelekeo wa kupatikana jina la mgombea wa urais kutokana na michakato inayoendelea ndani ya vyama hivyo.

No comments: