Thursday, February 19, 2015

COASTAL UNION WAIFUATA NDANDA MTWARA.




NA MWANDISHI WETU,TANGA.

TIMU ya Coastal Union ya Tanga imeondoka mkoani hapa leo asubuhi kuelekea mkoani 
Mtwara kwa ajili ya mechi yao ya Ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda SC itakayochezwa 
Jumamosi wiki hii.

Coastal Union ambayo mechi yao iliyopita dhidi ya Mbeya City iliyochezwa kwenye uwanja wa 
CCM Mkwakwani haikupata matokeo mazuri sana baada ya kulazimishwa sare hivo itaingia kwenye mechi hiyo mithili ya mbogo aliyejeruhiwa msituni

Akizungumzia maandalizi ya kuelekea mchezo huo,Kocha Mkuu wa Coastal Union,Mkenya 
James Nandwa alisema kuwa kikosi chake kimeimarika zaidi baada ya kuyafanyia kazi kwa 
asilimia kubwa mapungufu yaliyojitokeza mechi iliyopita.

Alisema kuwa dhamira yake kubwa ni kuhakikisha kikosi hicho kinaibuka na ushindi kwenye 
mchezo huo ambao unatazamiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na kila timu msimu huu 
kuonekana kujiimarisha vilivyo kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.

   "Kikosi changu kipo imara kuweza kuwakabili Ndanda SC ikiwemo kuhakikisha tunapata 
matokeo mazuri hii inatokana na maandalizi kabambe tuliyoyafanya hasa kubwa kurekebisha 
baadhi ya maeneo kwenye kikosi hiki "Alisema Kocha Nandwa.

Alisema kuwa mipango yake hivi sasa ni kukiwezesha kikosi cha timu hiyo kuweza kufanya 
vizuri kwenye mechi zao zijazo ili kuweza kusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa 
Ligi kuu hapa nchini.

Msafara wa Coastal Union uliondoka leo mkoani hapa kuelekea mkoani Mtwara unaongozwa 
na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ,Albert Peter ambapo baada ya kuwasili mkoani mtwara 
utafanya mazoezi.

No comments: