Sunday, February 15, 2015

CUF WATANGAZA RASMI KUANZA KUTOA FORM ZA WAGOMBEA WA NAFASI MBALIMBALI KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA HUU

Mkurugenzi wa Mipango, Uchaguzi na Bunge wa Chama cha Wananchi (CUF), Shaweji Mketo, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo
Chama cha wananchi CUF leo kimetangaza rasmi kuanza kwa mchakato wa  kura ya maoni kwa ajili ya kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya chama katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu,ambapo zoezi la kutoa form kwa wanachama wake wanaotaka nafasi mbalimbali kama nafasi ya madiwani,ubunge na pia nafasi ya urais wa Tanzania zimeanza kutolewa EXAUD MTEI ANAKUPA STORY YOTE
 
Akizungumza Kuanza kwa zoezi hilo mkurugenzi wa orgazation na uchaguzi wa chama hicho, Shaweji Mketo, amesema kuwa kwa sasa milango iko wazi kwa mwanachama yeyote mwenye sifa za kugombea uongozi ndani ya chama hicho kijitokeza kuchukua form kwani ni nafasi ya kipekee ya kuonyesha democrasia ndani ya chama hicho.

Akitaja gharama za kuchukua form ya kugombea nafasi mbalimbali amesema kuwa nafasi ya udiwani gharama ya form ni 10,000,nafasi ya ubunge ni 50,000 huku mgombea wa nafasi ya urais atachukua form kwa gharama ya shilingi laki tano.
 Mketo Amesema kuwa kuanza kwa zoezi hilo ndani ya chama haina maana kuwa ni kukiuka makubaliano umoja wa katiba ya wananchi UKAWA bali walichokubaliana ni kuwa kila mwanachama ahakikishe anatafuta wagombea wake na kisha kuwaweka pamoja kuangalia ni nani anafaa kuwa mgombea na kwa nafasi gani hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi kuhusu umoja huo kwani bado upo  imara na hauyumbi.

Katika  hatua nyingine chama cha wanachi cuf kimealamikia kuchezewa rafu na viongozi wa serikali kwa kulitumia jeshi la polisi vibaya ambapo amesema kuwa kuna baadhi wa viongozi wake wa mikoani ambao wamekuwa wakikamatwa na polisi na ndani kwa kile kinachoitwa ni kujihusisha na vitendo vya ugaidi ambapo amesema kuwa hizo ni mbinu chafu za kuwaponguza kasi viongozi hao baada ya kuona kuna uwezekano wa wao kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho na wanaweza kushinda nafasi hizo,majina ya viongozi hao waliokamatwa nimekuwekea mwisho wa story hii mdau wangu
TAMKO NZIMA HAPA





No comments: