Friday, February 13, 2015

HABARI NJEMA KWA WATUMIAJI WOTE WA UMEME TANZANIA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), Felix Ngamlagosi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo


MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA) imetangaza kushusha bei ya Umeme nchi nzima toka shilingi 257.3 kwa uniti moja hadi 251.70 kwa uniti moja  ni sawa na asilimia 2.21.Anaripoti KAROLI VINSENT.Endelea nayo.
         
Kushuka huko kwa Umeme imekuja siku chache kupita baada ya Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene kuitaka Mamlaka hiyo kushusha bei ya umeme kutokana na nishati ya Mafuta kushuka bei kwenye masoko mbalimbali hapa nchi na Duniani.
        
Akitangaza Bei hizo mpya za Umeme leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano na Waandishi Habari ,Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za nishati na Madini(EWURA) Felix Ngamlagosi ambapo amesema Mamlaka hiyo baada ya kuangalia vipengele vitatu ambavyo vinafanya umeme kupanda bei ikiwemo-
    
Bei ya Mafuta katika soko la dunia,hali ya shilingi ya kimarekani pamoja na mfumo wa gharama za umeme kwa ujumla wamebaini shirika la Umeme nchini TANESCO,linahaja ya kupunguza Umeme.
       
 Ngamlagosi amezitaja bei hizo mpya ni kwa wateja wenye matumizi ya kawaida  ambao wanaotumiza zaidi ya uniti 7o kwa mwezi,bei ya umeme itashuka kutoka  306 kwa uniti hadi 298 kwa uniti sawa na punguzo la shilingi 8.
       
 Na kwa wateja wanaotumia uniti 70 tu kwa mwenzi bei yao itabaki palepale ya shilingi 100 kwa uniti kama ilivyokuwa mwanzo.
           
Bwana Ngamsagosi alizitaja sehemu zingine ambazo ni  kwa wateja wa viwandani ambao wanatumiza zaidi ya Volti 4oo,kwa mwezi bei ya umeme imeshikuka kutoka shilingi 205 kwa uniti hadi 200 kwa uniti sawa na punguza la shilingi 4 kwa uniti,
              
  Mbali na hao wateja wengine ni wale waliounganishwa na msongo mkubwa wa umeme,bei ya umeme itashuka kutoka Shilingi 159 kwa uniti hadi 156 kwa uniti ambayo nao ni sawa na punguzo la shilingi 3 kwa uniti.
            
 Aidha,Bwana Ngamsagosi alisema Bei hizi zitaanza kutumika Rasmi tarehe moja ya mwezi wa tatu mwaka huu.
       
 Vilevile amesema kuwa bei hiyo ya umeme itapungua zaidi baada ya kukamilika kwa Bomba la gesi kutoka mtwala hadi Kinyerezi linalotarajia kumalizika mwezi wa sita mwaka huu,

Mbali na Bomba na Gesi Bwana Ngamsagosi alisema Shirika la Umeme Nchini Tanesco ambalo linatarajai kuzima mitambo yake yote ya mafuta ambayo ni ya dharula nayo pia itasaidia kushuka kwa umeme.

No comments: