Friday, February 20, 2015

KUHUSU KAFULILA NA MKOSAMALI KUHAMIA ACT TANZANIA



Baada ya kusambaa habari mbalimbali ambazo zilitangazwa na mmoja wa chama cha ACT Tanzania kuwa wabunge wawili wa kutoka chama cha NCCR mageuzi amba ni FELIX MKOSAMALI na DAVID KAFULILA watakihama chama hicho na kujiunga na ACT wabunge hao wameibuka leo na kutoa tamko kali.

Wakizugumza na wanahabari leo mapema katika ofisi za chama chao jijini Dar es salaam wabunge hao wamesema kuwa ni kweli kuwa wameziskia habari hizo katika magazeti mbalimbali ambazo zimesemwa na mmoja wa viongozi wa ACT lakini hazina ukweli na hazitakaa ziwe za ukweli kwani hawana muda wa kufanya jambo la ajabu kama hilo.

FELIX MKOSAMALI akizungumza kwa mshangao mkubwa amesema kuwa ni habari ambazo zinachekesha kuona chama kama ACT kinatumia majina yao kutaka kujitangaza kwani hakuna ukweli wa habari hizo.
“naomba nisema kitu kimoja naomba chama cha ACT watafute mbinu na njia nyingine ya kukikuza chama chao na sio njia hiyo wanayotumia kutumia majina ya wabunge kama sisi kujitangaza”alisema mkosamali

Aidha DAVID KAFULILA amesema kuwa yeye kama mwanachama wa nccr mageuzi na ukawa haoni haja ya kuhama kwani ukawa ni kimbilio la watanzania wengi hivyo kuhama ni sawa na kuchanganyikiwa na kukosa dira katika siasa.
Habari mbalimbali katika vyombo vya habari leo zilimnukuu kiongozi wa ACT kigoma akieleza kuwa wapo katika mazungumzo ya mwisho na wabunge hao kujiunga ndani ya chama hicho kipya.


No comments: