Tuesday, February 17, 2015

KUHUSU KUSHUSHWA KWA NAULI ZA DALA DALA NA MABASI YA MIKOANI


Chama cha kutetea abiria nchini Tanzania CHAKUA leo wameibuka na kuzitaka mamlaka husika kushusha nauli za mabasi ya mikoani na daladala mara moja kwa kile walichosema kuwa ni kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta duniani.EXAUD MTEI ANASIMULIA ZAID

Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam mwenyekiti wa chama hicho   HASSAN MCHANJAMA amesema kuwa mafuta yakipanda anayenufaika ni mmiliki wa vyombo vya usafiri kwa kupandisha nauli hivyo mafuta yakishuka hawana budi kushusha bei za nauli ili kumpunguzia mzigo mtumiaji ambaye ni mwananchi wa kawaida.

Amesema kuwa imekuwa ikitokea mafuta yakipanda kidogo tu wamiliki wa vyombo vya usafiri wamekuwa wakikimbilia kupandisha nauli mara moja lakini yanaposhuka wamekuwa wakikaa kimya kana kwamba hawajui kama yameshuka jambo ambalo ameliita ni kumkandamiza mwananchi wa kawaida ambaye ndiye abiria.

Amesma kuwa tayari chama cha kutetea abiria wamekwisha waandikia barua SUMATRA kwa lengo hilo na kuitaka iitishe mkutano na wadau ili wajadili jambo hilo lakini SUMATRA wamekuwa kimya jambo ambalo linaonyesha bado hawana nia njema kwa mtanzania wa kawaida.

Amesema kuwa CHAKUA inataka bei zote zipungue kwa asilimia 25 ambapo nauli za dala dala ambazo kwa sasa ni shilingi mia 400 ipungue na kufikia shilingi 300 na kwa upande wa mabasi yaendeyo mikoani mambo yawe hivyo hivyo ambapo mfano mabasi ambayo nauli ni shilingi elfu 40 bei hiyo ipungue na kufikia elfu 30 huku pia bei za usafiri wa majini zipungue kwa asilimia 25.

Amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri kuwa watapata hasara endepo watashusha bei ya nauli jambo ambalo amesema kuwa sio kweli na hakuna hasara yoyote watakayopata kwani ipo faida kubwa sana wanayopata kwani mafuta duniani imeshuka.


Aidha katika hatua nyingine chama hicho kimemtaka waziri wa uchukuzi mh SAMWELI SITA kuingilia kati swala hilo na kuagiza Sumatra washushe nauli mara moja ikiwa ni pamoja na kusikiliza kilio cha wadau mbalimbali kama ilivyokuwa mwaka 2009 baada ya mafuta kushuka bei.

No comments: