Saturday, February 14, 2015

MATOKEO YOTE YA KIDATO CHA NNE YAKO HAPA

Baraza la mitihani Tanzania NECTA leo mapema limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana,matokeo ambayo yaonyesha kuwa ufaulu nchini umeongezaka kwa asilimia 12.67 ambayio ni kutoka asilimia 57.09,ya mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 69.76 ya mwaka 2014.KAROL VICENT NA EXAUD MTEI WANARIPOTI

Akizungumza na wanahabari mapema leo katibu mkuu wa baraza hilo Dk CHARLES MSONDE mesema kuwa kupanda kwa kiwango hicho hicho cha ufaulu wa mitihani ni matokeo ya juhudi kubwa zinazofanywa na serikali katika kuboresha elimu nchini kupitia mpango wake wa matokeo makubwa sasa,pamoja na mpango wa serikali wa kuimarisha tathmini ya elimu katika mitihani ya kidato cha pili.

Katika matokeo hayo yanaonyesha kuwa jumla ya watahiniwa 196,805 sawa na asilimia 68.33 walifanya mtihani wa kidato cha nne 2014 wamefaulu huku wasichana wakiwa ni 89,845 sawa na asilimia 66.61 wakati wavulana waliofaulu ni 106,960 sawa na asilimia 69.85.

Watahiniwa wa shule waliofaulu ni 167643 sawa na asilimia 69.76 ya waliofanya mtihani,huku idadi ya wanafunzi wa kujitegemea waliofaulu ni 29,162 sawa na asilimia 61.693 ambapo mwaka 2013 jumla ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu ni 34,075 sawa na asilimia 66.23.

Aidha pia jumla ya watahiniwa wa mihani wa maarifa yani QT waliofaulu ni 6810 sawa na asilimia 55.29 tofauti na mwaka jana ambapo jumla ya waliofaulu ilikuwa 6529 sawa na asilimia 43.38.
 KWA ,MATOKEO YOTE SASA BONYEZA CHINI HAPO


Matokeo ya CSEE bofya hapa
Matokeo ya QT bofya hapa



No comments: