Friday, February 20, 2015

MWANAMITINDO TAUSI LIKOKOLA AWASILI NCHINI JIONI HII,TUKIO NZIMA LIKO HAPA

Mtanzania mwanamitindo mkongwe TAUSI LIKOKOLA akizngumza na wananchi mbalimbali waliojitokeza leo kumpokea katika uwanja wa ndege wa mwalimu julius myerere ambapo amewashukuru sana kuja kumpokea kwa wingi

Mwanamitndo maarufu nchini Tanzania ambaye amekuwa akifanya shughuli zake nchi za ujerumani na marekani TAUSI LIKOKOLA amerejea nchini baada ya kukaa nje ya Tanzania kwa Zaidi ya miaka 10 ambapo ameeleza mambo mbalimbali atakayoyafanya kipindi atakapokuwepo Tanzania.
Miss TANZANIA 2014 ndiye aliyeongoza mapokezi hayo jioni hii katika uwana wa ndege kumpokea mwanamitindo huyo mwenye makazi yake nchini marekani
Akizungumza na mtandao wa HABARI24 BLOG uliopiga kambi katika uwanja wa kimataifa wa mwalimu nyerere kusubiri ujio wake mrembo huyo ameueleza mtandao huu kuwa amefurajhi sana kuwa nchini Tanzania baada ya kipindi kirefu kuwa nje ya nchi ambapo amesema kuwa amejifunza mengi sana hasa katika fani hii ya wanamitindo.

Akizzngumza na baadhio ya wanahabari waliojitokeza kumpokea
TAUSI LIKOKOLA amesema kuwa fani ya uanamitindo nchini Tanzania bado ipo chini kwani bado hakuna uwekezaji mkubwa ambao unafanyika kuinua fani hiyo na kunachofanyika ni juhudi za mtu mmoja mmoja huku akitolea mfano kwa wanamitindo waliofaniiwa kama FLAVIAN MATATA kuwa wametumia juhudi binafsi kufikia hapo walipo.
Ngoma ndiyo asili ya mtanzania tucheze kidogo
Amesema kuwa ni lazima sasa watanzania na wadau mbalimbali kuelewa kuwa fani ya mitindo ni fani ambayo inaweza kuwasaidia vijana hivyo ni bora ikapewa kipaumbele na kuona inawasaidia vijana katika hali na mali.
TAUSI LIKOKOLA ambaye ni mmoja kati ya wanamitindo wa kwanza kabisa kufanikiwa kufanya kazi za mitindo kimataifa miaka ya 90 ambapo alifanikiwa kufanya kazi na makampuni makubwa ya marekani pia ni mwandishi wa vitabu mbalimbali amekuwa msaada mkubwa wa mawazo kwa wanamitindo wa kitanzania ambao wanafanya vizuri sasa kama FLAVIAN MATATA,MILLEN MAGESE,HERIETH PAUL na wengine wengi.
Mwanamitindo huyo ambaye amepokelea na aliyekuwa miss Tanzania bi SITTI MTEMVU atakuwa nchini Tanzania kwa siku kumi ambapo atafanya shughuli nyingi za kijamii ikiwemo kuzindua manukato yake mapya,kusaini vitabu vyake ambapo pia atakwenda visiwani zanzibari kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kijamiii kabla ya kurudi nchini marekani.
Mtandao wa HABARI24 BLOG upo sambamba kukueleza kila atakachokifanya katika ziara hiyo
PICHA ZINGINE ENDELEA CHINI


No comments: