Friday, February 20, 2015

NCCR MAGEUZI NAO WATANGAZA KUANZA MBIO ZA UCHAGUZI NDANI YA CHAMA

Katibu mkuu wa NCCR MAGEUZI ndugu MOSENA NYAMBABE akizngumza na wanahabari mapema leo kuhusu mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama hicho na utaratibu mzima wa kuchukua form za kuomba nafasi
Chama cha NCCR MASGEUZI leo kimetangaa rasmi kuanza mchakato wa uchaguzi ndani ya chama hicho ambapo kimetangaza  kuwaruhusu wanachama wa chama hicho kuchukua form za kuomba nafasi ya kugombea uongozi katika uchaguzi ujao mwishoni mwa mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari mapema leo katibu mkuu wa chama hicho MOSENA NYAMBABE amesema kuwa  utaratibbu wa umoja wa katiba ya wanacnhi UKAWA ni kuwa kila chama kitateua wagombea wake katika nafasi za udiwani,ubunge, na urais ambapo baadae watachujwa ili kupatikana wagombea wa UKAWA katika nafasi hizo
Akitaja ratiba ya uchukuaji wa form ndani ya chama hicho amesema kuwa kuanzia tarehe 15 hadi 30 mwezi wa tatu wanachama wanaotaka kuchukua form za udiwani wanaruhusiwa kuchukua form katika ofisi za kata mbalimbali zilizopo nchi nzima.


Na kuanzia tarehe 20 hadi tarehe 31 mwezi huu wa tatu wanaotaka kuchukua form za uwakilishi pamoja na ubunge ndani ya chama hicho wanatakiwa kuchukua form hizo katika ofisi za majimbo,na baadae wagombea wa nafasi ya uraisi wataanza kuchukua form kuanzia tarehe 1 hadi 30 ya mwezi wa  nne  kwa ajili ya kuomba nafasi ya kugombea nafasi hiyo.
Bwana mosena amesema kuwa wao kama chama wanaruhusu mtu yoyote ambaye ni mwanachama hai wa chama hicho na amekidhi vigezo kuja kuchukua form hizo hata kama amejiunga jana kwani baadae kutapita mchujo na kama ikionekana anafaa kukiwakilisha chama hicho jina lake litatua mezani kwa UKAWA kwa ajili ya mchujo.

Katika hatua nyingine chama hicho kimeeleza kutokuelewa zoezi alilolifanya RAISI KIKWETE la kubadilisha baadhi ya wakuu wa wilaya kwa kile alichokiita kuwa hawana kazi ya kufanya Zaidi ya kufanya kazi za chama tawala na kuwasaidia katika shughuli zao za kisiasa.
Mosena amesema kuwa kazi wanazofanya wakuu wa wilaya zinaweza kufanywa na wakurugenzi katika wilaya hivyo kuendelea kuwepo ka cheo hicho ni unyonyaji wa mali za watanzania huku nchi ikiendelea kuwa katika hali ya umaskini wa kupindukia.
“sisi tunaona ni muendelezo wa ccm na serikali kutengeneza mtandao wa kukilinda chama hicho kwani hatuoni kazi wanazofanya katika utendeji wa serikali”alisema mosena.
Aidha amesema kuwa ni kichekesho kuona watu  waliochaguliwa kwani hawana sifa za kuwa katika nafasi hiyo na inaonyesha kuwa ni jinsi gani rais ameidharau nafasi hiyo na kuamua kuwapa watu ili kuwalipa fadhila.



No comments: