Thursday, February 12, 2015

USIIKOSE HII KUTOKA DAR ES SALAAM LEO


Mwenyekiti wa CHADEMA,Mh. Freeman Mbowe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha ACT,Ndg. Samson Mwigamba.
Sehemu ya Viongozi wa Vyama vya Siasa waliohudhulia Mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva (hayupo pichani) leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Francis Mutungi akichangia mada katika mkutano huo wa Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha UDP,Mh. John Momose Cheyo akiwa na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Ndg. Nape Nnauye wakati wa mapumziko mafupi ya mkutano huo.

Eeehh....bwanaaaaa upoooo........?? Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi,Mh. James Mbatia akifurahi jambo na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Ndg. Nape Nnauye.Katikati ni Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dkt. Wilbroad Slaa.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii


 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Damian Lubuva akizungumza wakati wa mkutano na Viongozi wa Vyama vya Siasa uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte,Jijini Dar es salaam.Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Julius Malaba na kulia ni Kamishina wa Tume yaTaifa ya Uchaguzi,Prof. Amon Challigha

TUTAENDELEA KUPATA MAONI
KATIKA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA-JAJI LUBUVA


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema itaendelea
kupata maoni kwa wadau juu ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura kwa kutumia
mfumo mpya  wa uchukuaji wa alama za
vidole kwa kutumia BVR ili kurahisisha wapiga kura.


Hayo ameyasema leo  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC),Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakati alipokutana na viongozi wa vyama vya siasa
na wadau wengine jijini Dar es Salaam ,Lubuva amesema mfumo wa uandikishaji wa
daftari la wapiga kura ni mpya hivyo ni lazima Tume itoe  taarifa mara kwa mara na kupata mawazo mengine katika uboreshaji wa daftari hilo.


Lubuva amesema daftari la wapiga kura limekuwa na
malalamiko mengi kwa vyama vya siasa na kuona haja ya kubadili mfumo wa
uandikishaji kwa kuchukua alama za vidole kwa kutumia kifaa cha BVR ili kuondokana na malalamiko hayo.


“Tume inafanya kazi kwa kujitegemea hakuna mtu yeyote
anaweza kuipangia majukumu na hata mkutano wetu wa leo sio shinikizo la Mbunge
wa chama chochote kwani hii ni tume huru”amesma Jaji Lubuva.


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi -CCM (Taifa) ,Nape
Nnauye amesema Tume imekuwa ikikaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa taarifa na
kuwa na shaka kutokana na masuala yaliyopo katika tume ni mazito ikiwemo
uboreshaji wa daftari la wapiga kura ambalo linatakiwa litumike katika kura ya
maoni pamoja na uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.


Amesema kama chama tawala wanataka kuona masuala haya
yanawekwa wazi na tume mara kwa mara ili wananchi wawe tayari katika
kuandikishwa katika daftari hilo.

No comments: