Wananchi wa maeneo ya vingunguti wakifurahi pamoja na kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam mara baada ya uzinduzi wa kituo hicho cha polisi leo |
Kamishna SULEMAN KOVA akiwa na mdau ambaye ndiye aliyejengenga kituo hicho IMTIYAZ ABBAS wakizindua rasmi kituo hicho |
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam leo
wamezindua kituo kipya cha polisi kilichopo vingunguti jijini Dare s salaam
ikiwa ni hatua ya kupambana na makundi ya wahalifu katika maeneo hayo ambayo
yamekuwa sugu kwa sasa.
Kituo hicho ambacho kina uwezo wa kuhudumia zaidi ya
wananchi million moja kimejengwa na mzalendo mkazi wa maeneo hayo IMTIYAZI
ABBAS kituo ambacho kimegharimu zaidi ya shilingi za kitanzania million 56 hadi
kumamilika kwake.
Akizungumza wakati wa kuzindua kituo hicho kamishna
wa kanda maaluim ya Dar es salaam SULEMAN KOVA amesema kuwa kuwepo kwa kituo
hicho saa ni ishara tosha kuwa uhalifu katika maeneo hayo umefikia tamati kwani
kituo hicho kitakuwa na askari wa kutosha kuwahudumia wananchi wa maeneo hayo
na viunga vyake.
“sasa muda
umefika wa wezi na wakabaji kutafuta kazi zingine za kufanya katika maeneo haya
kwani tumejipanga kuhakikisha kuwa hakuna mhalifu atakayeishi katika maeneo
haya,bora atafute kazi nyingine ya kufanya kama kulima kuliko kuendelea kuwa
mhalifu”alisema kova
Kamishna kova amesema kuwa ni muda mrefu sasa wananchi
wa maeneo hayo ya vingunguti wamekuwa wakilia kwa kukosa kituo bora cha polisi
na sasa muda umefikia na wamepata kituo hicho sasa kilichobaki ni kushirikiana
na wananchi kuwafichua wahalifu katika maeneo hayo.
Aidha amemshukuru mtanzania mzalendo ambaye ndiye
aliyejitoa kwa pesa kujenga kituo hicho ambapo kamishna kova amewaomba
watanzania wengine wazalendo kujitkeza kujenga vituo vya polisi ili kuwasaidia
wanachi kupata usalama zaidi.
Aidha bwana ABBAS ambaye ndiye aliyejenga kituo
hicho ameahidi kukiboresha zaidi ikiwa ni pamoja na kununua vifaa vya kisasa
ili kuwasaidia askari katika kupambana na wahalifu.
Nao wanachi wa maeneo hayo ya vingunguti wameonyesha
furaha yao baada ya kupata kituo hicho baada ya kukiriokuwa kumekuwa na
wahalifu wengi sana katika maeneo hayo lakini ujio wa kituo hicho katika maeneo
yao kitasaidia kupunguza uhalifu uliokithiri kttika maeneo hayo.
PICHA NYINGINE ZAIDI ZIKO CHINI
No comments:
Post a Comment