Mwenyekiti wa jumuiya ya vijana ya chama cha wanachi CUF(juvicuf) HAMIDU BOBANI akizngumza na wanahabari kuhusu maandano hayo ya kesho |
Jumuiya ya vijana ya chama cha wananchi CUF (JUVICUF)
leo wametangaza kufanya maandamano ya Amani siku ya kesho ijumaa maandamano
ambayo yataanzia katika maeneo ya buguruni na kuelekea katika ofisi za wizara
ya mambo ya ndani na baadae kuelekea tume ya taifa uchaguzi Tanzania.
Akizungumza na wanahabari mapema leo mwenyekiti wa
jumuiya hiyo HAMIDU BOBAN amesema kuwa maandamano hayo yana lengo la kupinga na
kulaani vikali nguvu na uvunjaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi la polisi
lakini pia lengo lingine ni kufikisha malalamiko yao kwenye tume ya uchaguzi
juu ya uchache wa siku zilizowekwa za uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga
kura.
Amesema kuwa jumiya hiyo ilipeleka ombi la kufanyika
kwa maandamano hayo jeshi la polisi lakini cha kushangaza ni kuwa viongozi wao
waliitwa na polisi na kuambiwa kuwa haiwezekani kufanyika kwa maandamano hayo
kwa sababu kuwa watasababisha usumbufu kwa wananchi wa kawaida ambao watakuwa
katika shughuli zao jambo ambalo mwenyikiti huyo amesema kuwa sio sababu ya
kutosha ya kufanya maandamanop hayo yasiwepo.
Amesema kuwa pamoja na jeshi la polisi kupiga marufuku
maandamano hayo wao kama chama wanatangaza kuwa maandano hayo yapo kama kawaida
na hakuna mtu wa kuyazuia na watafanya maandanao ya Amani lakini kama polisi
wataanzisha vurugu wao watatumia njia za kujihami jambo ambalo litazua vurugu Zaidi.
Maandanamo hayo ambayo yataongozwa na waziri wa
miundombini na uchukuzi wa serikali ya umoja wa kitaifa zanzibari mh JUMA DUNI
HAJI ambaye tayari yupo jijini Dar kwa ajili ya maandano hayo wamepanga kuanza
mnamo saa nne kamili asubuhi ambapo mwenyikiti huyo amewataka vijana wa chama
chake kujitokea kwa wingi katika maandanao hayo.
KOVA APIGA MARUFUKU
Kamishna wa polisi kanda maalum Dar es salaam SULEMAN KOVA akizungumza na wanabari muda huu kupiga marufuku maandano hayo. |
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam kupitia
kamishina wa kanda hiyo SULEMANI KOVA limatangaza kuzuia maandamano yaliyopangwa
kufanywa na jumuiya ya vijana ya chama cha wananchi cuf kwa kile walichodai
kuwa sababu za kufanyika kwa maandamano hayo hazitoshi na badala yake itakuwa
ni mbinu ya kuvuruga Amani katika jiji la Dar es salaam
Akizungumza na wanahabari masaa machache baada ya
vijana wa CUF kutangaza kuwepo kwa maandamano hayo kamishna KOVA amesema kuwa
maandamano hayo sio halali na hayana Baraka za polisi hivyo wananchi
wasidanganyike kutoka kwani yanaweza kuwakuta makubwa na wasipate wa
kuimlalamikia.
Amesema kuwa sababu zilizotolewa za kufanya maandanao
hayo ni sababu ambazo zinajadilika hata bila maandanao hivyo haoni haja ya
kufanya maandano hayo na badala yake akawashauri vijana hao kutafuta njia nyingine
ya kuwasilisha malalamiko yao na sio kuandamana.
“Mimi nasema hakuna maandamano kesho na nashauri mtu
yeyote asitoke kuandama kwa maana yatakayomkuta asije akamlaumu mtu atajikuta
yupo sero bila sababu ya msingi,bora hawa vijana wakae majumbani kwao watafute
njia nyingine za kufikisha maoni yao”amesema kova
Kamishna KOVA amesema kuwa polisi wamezuia maandamano
hayo kwa nia nzuri chini ya kifungu cha 43(1-6) cha sheria ya polisi na polisi
wasaidizi sura ya 322 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.
Aidha amesema kuwa kutokana na taarifa kuwa vijana hao
wa CUF bado wanazidi kuhamasishana kufanya maandamano hayo inaonyesha wazi kuwa
lengo ni uvunjifu wa Amani hivyo polisi watatumia uwezo wake wote hapo kesho
kuhakikisha kuwa wanazima maandano hayo.
No comments:
Post a Comment