Wednesday, March 18, 2015

EU WAMPA TUZO MAMA HELEN KIJO BISIMBA

Umoja wa Ulaya umemtunuku Mama Helen Kijo- Bissimba kutokana na mchango wake kwa ajili ya kutetea na kulinda haki za binadamu nchiini.

           Tuzo hiyo, ilitolewa jana na EU siku ya Jumanne wiki hii jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mwaka  wa Maendeleo Ulaya  2015.

Balozi wa Umoja wa Ulaya bwana Filberto Sebregondi alitoa tuzo hizo na kusema kuwa lengo lake ni kusimamia haki kwenye masuala ya kiulimwengu ikiwemo  kupambana na umasikini na kuhamasisha raia kujihusisha na maendeleo.
Wengine waliotunukiwa tuzo katika hafla hiyo pamoja na Mama Bissimba ni wanamziki

Keisha Saban,  Fareed Kubanda (FID Q),  na Balozi Mpungwe, pamona na Paul Ndunguru ambae ni msanii na  mchoraji.
EU imekuwa mstari wa mbele kupambana na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu hususani ukatili dhidi ya Wanawake na watoto ikiwemo vitendo vya ukeketaji, ndoa za utotoni, na mauaji ya vikongwe.

Vilevile, EU imekuwa mstari wa mbele kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na kupinga adhabu ya kifo.

No comments: