Friday, March 20, 2015

KIMENUKA UKAWA TEMEKE,CHADEMA WASEMA HATUWAPI CUF JIMBO KAMA PIPI.SOMA HAPA

Wakati toka juzi kukienea taarifa  kuwa tayari umoja wa katiba ukawa umemaliza kazi ya kugawana majimbo ya uchaguzi katika mkoa wa Dar es salaam na kuwa tayari kila mtu ameshapata jimbo lake,chama cha democrasia na maendeleo chadema mkoa wa temeke leo kimekanusha maneno yaliyoenezwa kuwa tayari jimbo hilo wameshapewa chama cha CUF .


Akizugumza na wanahabari leo mwenyekiti mh BERNARD MWAKYEMBE kwa niaba ya kamati tendaji ya jimbo hilo amesema kuwa jimbo haligawiwi kama pipi kwani wanaamini kuwa viongozi wa UKAWA watatoa mwongozo ambaop kila chama kitatoa mgombea na baada ya hapo kutakuwa na kura ya maoni pamoja na kuchagua mgombea na baada ya hapo anayekubalika napande zote atapewa nafasi ya kugombea katika jimbo hilo.amesema kuwa habari ambazo zimeenezwa na magazeti leo kuwa jimbo hilo limepewa CUF ni uzushi na uhuni mkubwa


No comments: