Monday, March 23, 2015

TAARIFA MBILI KUTOKA TFF ASUBUHI HII


         Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini –TFF Bw. Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia (The She-polopolo).

Katika salam zake Rais Malinzi amesema ushindi walioupata Twiga Stars katika mchezo huo wa awali, umetokana na maandalizi mazuri waliyoyapata chini ya kocha mkuu Rogasian Kaijage, benchi lake la ufundi na TFF.

Aidha Rais amewataka Twiga Stars kutobweteka kwa ushindi huo wa awali walioupata, bali wanapaswa kujiandaa vizuri zaidi kwa ajili ya mchezo wa marudiano ili waweze kupata ushindi na kuipeperusha vuzuri bendera ya Taifa ya Tanzania.
Mchezo wa marduiano unatarajiwa kufanyika kati ya April 10,11 na 12, 2015, huu jijini Dar es alaam na mshindi wa jumla atafuzu moja kwa moja kwenye fainali za Afrika kwa Soka la Wanawake (All Africa Games Women)  zitakazofanyika Brazzavile Congo Septemba 3-18 mwaka huu.

Twiga Stars inatarajiwa kuwasili saa 7 kamili usiku (jumanne) jijini Dar es salaam kwa usafiri wa Shirika la Ndege la Ethiopia ikitokea nchini Zambia.
Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu , Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), watanzania wote wanawapa pongezi  Twiga Stars kwa ushindi walioupata wa awali na kuwatakia maandalizi mema ya mchezo wa marudaiano.

Mabao ya Twiga Stars katika mchezo wa jana dhidi ya Zambia (The She-polopolo) yalifungwa na Asha Rashid (2), Shelder Boniface (1) na Sophia Mwasikili (1).
                                        
                      BEACH SOCCER YAREJEA LEO                                       
Wakati huo timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer) inarejea leo mchana saa 8:45, kwa Shirika la Ndege la Ethiopia ikitokea nchini Misri ambapo jana ilipoteza mchezo wake wa marudiano kwa kufungwa 9-4 na wenyeji.
Rais Malinzi amesema timu ya Soka la Ufukweni haikupata matokeo mazuri katika mchezo wake kutokana na ugeni wa michuano hiyo, uzoefu ndio ulikuwa kikwazo kwa timu ya Tanzania, kwani ndio mara ya kwanza kushiriki michuano hiyo ikiwa ni miezi sita tangu kutambulishwa kwa mchezo huo nchini Tanzania.
Ili kuwa na timu bora ya Taifa na wachezaji wengi wa mchezo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limepanga kuutangaza na kuufundisha mpira wa ufukweni katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania, tofauti na sasa ambapo mchezo huo unachezwa  Dar es salaam na Zanzibar.
Katika mchezo wa jana mabao ya Tanzania yalifungwa na Ally Rabbi (3) Kashiru Salum (1), Tanzania imetolewa kuwania kufuzu kwa fainali za Soka la Ufukweni barani Afrika na Misri kwa jumla ya mabao 15-6.
Misri imefanikiwa kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa Soka la Ufukweni Visiwa vya Shelisheli, zitakazofanyika mwezi April mwaka huu kwa mara ya saba mfululizo tangu kuanzishwa kwa mchezo huo mwaka 2006 nchini humo.


No comments: