Thursday, April 16, 2015

MADIWANI MANISPAA YA TEMEKE WAFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA MANISPAA YAO.PICHA ZIKO HAPA

Madiwani wa manispaa ya Temeke leo wamekagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo na kijamii inayoendelea katika manispaa hiyo ikiwemo maabara,madarasa na nyumba za walimu.


Akizungumza na wanahabari diwani wa kata ya somangira AISHA MPINJILA amesema kuwa kukamilishwa kwa miradi hiyo kwa asilimia 99 kutasaidia kuinua kiwango cha elimu katika manispaa hiyo na kwa nchi kwa ujumla.



Aidha kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Temeke WAZIRI KOMBO amewataka wanafunzi katika manispaa hiyo kuchagua michepuo ya sayansi kwani ndio mchepuo wenye suluhisho la ajira kwa sasa nchini huku akiwataka wanafunzi na walimu kutunza miradi hiyo. Baadhi ya shule ambazo zimetembelewa  ni Pemba mnanz secondary,nguva secondary,kidete secondary,kimbiji secondary  
PICHA NYINGINE ZA ZIARA HIYO ZIPO CHINI







No comments: