Wednesday, April 15, 2015

VIONGOZI WA COASTAL UNION WATAKIWA KUSHIKAMANA.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal
Union,Akida Machai akimuelezea mikakati ya timu hiyo mkuu wa Mkoa wa
Tanga Magalula Saidi wakati wa kikao cha pamoja baina ya viongozi wa
Coastal Union na Mkuu huyo wa mkoa kwa lengo la kufahamiana
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Magalula Saidi katikati
waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Coastal Union na
viongozi wa mkoa,kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Coastal
Union,Steven Mguto
NA MWANDISHI WETU,TANGA.

VIONGOZI wa Klabu ya Coastal Union wamewatakiwa kushikamana vilivyo
ili kuweza kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika michezo yao
iliyosalia katika Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania Bara.

Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Magalula Saidi wakati
alipokutana na viongozi wa timu hiyo ofisini kwa lengo la kufahamiana
ambapo Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto aliwaongozwa
viongozi wengine kwenye kikao hicho.

Alisema kuwa muda uliobakia kwenye mechi za Ligi kuu sio wa kuanza
kufikiria ni kitu gani kimetokea bali ni kuweka mipango imara na
madhubuti itakayowapa mafanikio ili waweze kujipanga msimu ujao kwa
ligi nyengine.

Aidha aliwataka viongozi hao kujiepusha na migogoro, mifarakano
iliyokuwa na tija kwani hali hiyo ikiruhusiwa itashindwa kuwapa
maendeleo na kukwamisha mipango yao waliojiwekea.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto
alimuhaidi mkuu wa mkoa huyo kuyafanyia kazi kwa asilimia kubwa
maelekezo aliyoyatoa ili waweze kupata mafanikio..

Naye, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Coastal Union, Akida Machai
alisema changamoto zilizojitokeza kwenye michuano hiyo watazifanyia
kazi kwa umakini mkubwa ili ziweze kuleta ufanisi katika michezo
iliyosalia.

Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa soka akiwemo
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho la soka Nchini (TFF) Khalid
Abdallah.

No comments: