Wednesday, July 15, 2015

CUF WAIBUKA MUDA HUU NA KUTOA YA MOYONI JUU YA UKAWA,TIZAMA HII

Viongozi wa chama cha wananchi CUF wakiongiozwa na mama MAGDALENA SAKAYA ambaye ni naibu katibu mkuu wa chama hicho wakijitokeza mbele ya wanahabari leo
 Baada ya jana kuzagaa habari mbalimbali zikielezea kuwa chama cha wananchi CUF kimejiondoa katika ndoa ya muungano wa umoja wa  katiba ya wanahanchi UKAWA,viongozi wa chama hicho leo wameibuka na kutoa utetezi juu ya swala hilo.SHUGHUDA WAKO EXAUD MTEI ANAELEZA ZAIDI----------
Katika hali isiyokuwa ya kawaida jana katika mkutano wa umoja huo uliofanyika katika ukumbi  mmoja jijini Dar es salaam ulishughudia mkutano huo kuendelea huku kukiwa hakuna uwakilishi wa chama cha wananchi CUF jambo ambalo lilizua mijadala kila kona kuwa umoja huo umevunjika rasmi na chama hicho kimejiondoa katika ndoa hiyo.
Mapema leo jijini dare s salaam katika mkutano uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama hicho baina ya viongozi wa chama na wanahabari,Naibu katibu mkuu wa chama hicho mama MAGDALENA SAKAYA amewaeleza wanahabari kuwa ni kweli kuwa chama chao hakikuweza kushiriki katika mkutano wa jana kwa kile alichojitetea kuwa sababu za kikatiba ndani ya chama hicho na kwa kuwa kuna maamuzi makubwa ya kinchi yanayoendelea baina ya umoja huo wameona ni muda sasa wa kuita mkutano wa baraza kuu la chama hicho kwa dharura kushauriana mambo kadhaa kabla ya kuuendelea na ndoa hiyo ya vyama vinne.


“Baada ya kikao cha ukawa cha terehe 11,mwezi wa saba viongozi wa chama chetu akiwemo mwenyekiti wa chama,naibu katibu mkuu na wakurugenzi tumekuwa na vikao vyetu vya ndani kwa lengo la kuweka mambo flani sawa kabla ya kuamua,na ndiyo maana jana hatukuweza kuonekana katika mkutano huo”amesema SAKAYA
Amesema kuwa kutokuhudhuria kwa kikao cha jana tarehe 14 kilichokuwa kinatajwa kuwa ndio kitatoa mgombea wa umoja huo haina maana kuwa chama hicho kimesusia umoja huo na kuongeza kuwa hawawezi kufanya hivyo kwa kuwa hata jina na maana ya umoja huo umeasisiwa na kiongozi wa chama hicho profesa lipumba.
Chama hicho kimeamua kuita mkutano wa baraza kuu wa dharura terehe 25 mwezi huu kujadiliana maswala maalum likiwemo la ushiriki wao ndani ya ukawa na baada ya hapo ndiyo watajua kama wanaendelea na ndoa hiyo ama imekufa
Katika hali ambayo imezua maswali mengi naye Mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama hicho bwana ABDUL KAMBAYA amesema kuwa viongozi wa chama hicho akiwemo mweyekiti wa chama hicho hawakuwa na taarifa yoyote ya mkutano wa ukawa jana tarehe 14  huku akisema kuwa mwenyekiti wa chama hicho alipokea ujumbe wa kualikwa katika mkutano huo jana saa tatu jambo ambalo lilimwia ngumu yeye kuamua kufika kwake.
“Ni kweli kuwa kikao cha mwisho cha ukawa kilitangaza kuwa tarehe 14 ndiyo tutamtoa mwali wetu wa urais na mh LIPUMBA alikuwepo,lakini katibu wetu wa ukawa ambaye ni DK SLAA ndiye mwenye jukumu la kutoa taarifa kwa chama kuwa mkutano huo ni wapi unafanyika mapema ili kiongozi wetu aweze kufika lakiini taarifa haikutufikia kwa wakati na ndio sababu nyingine ya sisi kushindwa kufika jana”Ameeleza kambaya.
Aidha kambaya amesema kuwa sababu nyingine iliyowafanya viongozi wa CUF kujitoa kwanza katika mchakato huo ni kile kinachoitwa kudharaulika kwa mwenyekiti wao,amesema kuwa ilikubalika kuwa tarehe 14 ndiyo angetangazwa mgombea wa ukawa lakini cha kusikitisha sana terehe 12 tayari kuna vyombo vya habari vilikuwa vinamtangaza mgombea wa umoja huo na vyombo vingine vya habari vikienda mbali hadi kutaja kura aliopata katika mchakato huo.
Amesema kuwa hali hiyo imeamsha jazba na hasira baina ya viongozi na wanachama wa chama hicho chenye maskani yake buguruni Dar es salaam na kuamua kusitisha kwanza ushiriki wao katika mchakato huo na kurudi kwa wanachama na viongozi kuchukua ushauri wao kabla ya kuamua jambo la kufanya.
Akizngumzia kile ambacho kilizngumzwa jana mna mwenyekiti mwenza wa mkawa JAMES MBATIA kuwa umo9ja huo tayari wameshampata mgombea wa uraisi na muda wowote watamtaja --------amesema kuwa swala la urais ndani ya ukawa sio jambo kubwa sana kwa kuwa sifa za mgombea wanayemtaka wameshaziweka wazi hivyo ni kama ameshapatikana ila swala kubwa ni maridhiano na umoja ndani ya umoja huo


No comments: