Saturday, July 25, 2015

HAWAVUMI LAKINI WAMO--HAMAD RASHID LEO NA CHAMA CHAKE KIPYA,ATUMA SALAAM NEC

HAMAD RASHID akisalimiana na wanachama wa chama cha Alliance for Democtratic Change (ADC) wakati akiwasili katika mkutano huo 

 Aliyekuwa mbunge wa jimbo la wawi Zanzibar kupitia chama cha wananchi CUF ambaye hivi majuzi ametangaza kukiahama chama hicho na kujiunga na chama kipya cha ADC Mh HAMAD RASHID ameitaka Tume ya Taifa ya uchaguzi kufanya kila njia kuhakikisha kuwa watanzania wote wenye sifa za kupiga kura wanajiandikisha ili waweze kutimiza haki yao hiyo ya msingi.EXAUD MTEI anasimulia----
Wanachama wa Alliance for Democtratic Change (ADC) wakiwa katika mkutano huo
Kauli hiyo imekuja wakati zoezi la uandikishwaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura likiwa linaendelea katika mkoa wa Dar es salaam ambapo limezua gumzo kubwa kutokana na kasoro mbalimbali ambazo zinaonekana kujitokeza katika zoezi hilo jambo ambalo linalalamikiwa na wadau wa maswala ya siasa kuwa linaweza kuwanyima watanzania wengi haki yao ya msingi ya kupiga kura.
Naibu Katibu Mkuu, Doyo Hassan Doyo akimkabidhi form ya kuomba ridhaa ya cha kwa ajili ya kugombea nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndugu ABUBAKAR RAKESH ambaye pia ni mlemavu wa miguu 
Hamad Rashid ametoa kauli hiyo mapema leo wakati wa zoezi la uchukuaji wa form za kuomba ridhaa ya chama hicho kipya ya kuwania nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ambapo wanachama mbalimbali wamejitokeza kuiwania nafasi hiyo.

Mh Hamad amesema kuwa haki ya kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya kila mtanzania mwenye kutimiza vigezo hivyo lazima tume ifanye kila njia kuhakikisha kuwa hakuna mtanzania anayeachwa nyuma kutokana nna sababu yoyote kwani kama watanzania watakosa haki ya kupiga kura watakuwa wamekosa haki ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Aanayekabudhiwa form hapa ni aliyewahi kuwa mgombea wa kiti cha uenyekiti wa chama cha wananchi CUFChifu Yemba naye anaomba nafasi ya kugombea urais wa Tanzania
Aidha akizngumza na wagombea mbalimbali waliojitokeza kuchukua form pamoja na wanachama wa chama hicho ambacho kinajinasibu kuwasaidia watanzania hasa wa hali ya chini amesema kuwa ni muda wa watanzania kuchagua viongozi bila kujali aina au maumbili ya mgombea kwani hata walemavu wana haki ya kuchagua na kuchaguliwa hivyo chama cha ADC kimekuwa kikiwapa watanzania wote nafasi bila kujali mapungufu yao.

Katika hatua nyingine mtandao huu umedokezwa kuwa mh Hamad Rashid anataraji kuchukua form ya kuomba ridhaa ya chama hicho kuwania nafasi ya urais huko Zanzibar.

No comments: