Friday, July 3, 2015

Klabu ya Simba yashirikiana na Tigo Tanzania kuzindua huduma ya Simba news.

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakisikiliza hotuba ya Meneja Mawasiliano ya Biashara wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Jacqueline Nnunduma, wakati wa uzinduzi wa huduma ya Simba News kwa ajili ya kupata habari za klabu hiyo

Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva (kulia), akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika uzinduzi wa huduma ya Simba News iliyozunduliwa kwa ushirikiano wa Tigo na Simba, kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG Group LTD, Iman Kajula.

Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa huduma ya Simba News kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, kulia ni Meneja Mawasiliano ya Biashara wa Tigo Jacqueline Nnunduma na kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG Group LTD Iman Kajula.

Meneja Mawasiliano ya Biashara wa Tigo Jacqueline Nnunduma, (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya Simba News uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Rais wa Simba Evans Aveva na kushoto ni Mkurugenzi wa EAG Group LTD, Iman Kajula ambaye ni Mshauri wa kutekeleza shughuli za Kibiashara na Masoko katika Klabu ya Simba.

 Kampuni ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na klabu ya mpira wa miguu ya Simba wamezindua huduma ya ujumbe mfupi ijulikanayo kama 'Simba SMS', ambayo lengo lake nikuwapatia wateja wa Tigo taarifa zinazoihusu klabu ya Simba popote walipo nchini.
Huduma hii mpya inajulikana kama 'SIMBA SMS'. Njia hii ni rahisi na yenye ufanisi yenye kuifanya dunia ijulikane kwa wateja wake. "Pamoja na kasi yaukuaji wa Tehama, Tigo inaelewa umuhimu wakutoa taarifa kwa wateja wake, ndiyo maana leo, tunajisikia fahari kuzindua huduma hii iliyotengenezwa vizuri ya SIMBA SMS nawashirika wetu wa klabu ya SIMBA pamoja na Premier Mobile Solutions (PMS), ilikuendelea kuwapa wateja wetu taarifa zinazohusu masuala ya sasa huku wakifurahia habari mpya zinazohusu klabu,"alisema meneja wa mawasiliano ya kibiashara Jacqueline Nnunduma.

Lengo letu si tukuwapatia wateja wetu taarifa kiurahisi zaidi, lakini pia kuwapatia taarifa hizo kwa wakati na zenye uhakika kutoka vyanzo vya michezo vyenye kuaminika," aliongeza Nnunduma.
Akizungumza kwa niaba ya Klabu ya Simba,Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva alisema, "Tunaamini ubunifu huu bila shaka utawawezesha mashabiki wote wa Simba na wa soka kwa ujumla ambao pia ni wateja wa Tigo kupata habari mbalimbali za klabu ya Simba kupitia simu zao za mkononi”.

Tunawahimiza mashabiki wetu kujiunga na huduma hii kupitia Tigo ili waweze kupata nakufurahia habari mbalimbali kutoka klabu ya Simba. Aliendelea Aveva.

Akiongea katika tukio hilo Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya EAG Group LTD Imani Kajula ambae ni mshauri wa kutekeleza shughli za kibiashara na masoko katika klabu ya Simba, alisema “Tunatarajia kuendelea kuwapatia mashabiki wa Simba huduma za kisasa kwa kutumia teknolojia zisizokuwa na usumbufu wa aina yeyote  kupitia wadau wanaoaminika ndani ya Tanzania”

Kwa upande  wake Meneja Uendeshaji wa Premier Mobile Solutions, Bi Lulu Ramole alisema kuwa huduma hii imetengenezwa ili kuwawezesha wateja kupata habari za papo kwa papo naaliongeza kuwa huduma ipo katika mfumo wa vifurushi vya Combo / BUNDLE PACK ambapo wateja wa Tigo watakuwa wakilipia mara moja kwa siku na kupokea kiwango cha chini cha  habari nne (04) na habari mpya za kila siku zina zohusu klabu ya Simba.
Huduma pia itamruhusu mteja aliyejiunga kujitoa kwenye huduma hii wakati wowote akitaka bila vikwazo vyovyote na pia kwenye huduma hii kutakuwepo na neon kuu “MSAADA”kwa ajili ya kusaidia juu ya maswali mbalimbali ya nayo ulizwa mara kwa mara na wateja wakati wakifurahia huduma.
Ili  kujiunga na huduma hizi unatakiwa kutuma neon kuu SIMBA kwenda 15460. Utakapo jiunga tu mteja atapokea habari kutokana na neon analolituma kila siku na atatozwa kiasi cha shilingi za kitanzania 150 kwa siku. Na ili kujitoa kwenye huduma mteja atahitaji kutuma neno ONDOA SIMBA kwenda 15,460.
 

No comments: