Tuesday, July 21, 2015

KUBWA--BAADA YA LEMBELI KUJILIPUA LEO,SOMA HII ILIYOTOKA HUKO CHADEMA MUDA MFUPI TENA



Mbunge machachari wa Kahama James Lembeli ametangaza rasmi kujivua uanachama wa CCM na kujiunga na CHADEMA katika mkutano na waandishi wa habari unaoendelea hapa DSM.

Tukio hili pia limeshatangazwa live na Radio one stereo.Ikumbukwe mbunge huyu mpambanaji dhidi ya ufisadi ndiye aliyeongoza kamati teule ya bunge iliyoshughulikia suala la operesheni tokomeza na kusababisha mawaziri wanne kujiuzulu. 
Mbunge Wa Kahama(CCM) ametangaza rasmi kwamba atagombea Ubunge Katika jimbo la Kahama kwa Tiketi ya CHADEMA,


Baada ya tukio hilo la mbunge LEMBELI tangaza kujiunga na CCM uongozi wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA kupitia kwa msema ji wa cha ahicho akaibuka na kauli nyingine ya kuwashtua watu juu ya hamisha hamisha hiyo inayoendelea.akaweka kauli hii kwenye mitandao


Tumemaliza event ya kwanza leo. Mhe. James Lembeli baada ya kuwa CCM kimwili kwa muda mrefu huku dhamira yake, uwezo wake, akili zake, zikiwa Kwenye mabadiliko ya kweli, leo kaamua kuuhamisha kabisa na mwili huo. Kuanzia Julai 21 amekamilisha kile ambacho akili yake kilikuwa kinahitaji. Amejiunga na wapiganaji wa CHADEMA.
Hiyo ya kwanza. Kesho tutawapiga kiaina tena. Keshokutwa pia. Halikadhalika mtondo bila kusahau mtondogoo! Mind you, it would be in different styles and different places.
Hakuna jiwe litabaki bila kugeuzwa kabla CCM haijaondoka madarakani mwaka huu. Ukiona Simba kanyeshewa usidhani paka. Ukiona Kobe kainama ujue anatunga Sheria.
Ukimya umeanza kuja na kishindo kikubwa. Tuko tayari. Tuonane kesho kwa masaa 3. Hitting them again.
Wametangulia na kufuli na dawa ya kufuli ni ufunguo.






Baaya ya kauli hiyo kumeibuka za chini chini kuwa aliyekuwa mbunge wa viti maalum wa CCM  Ester Bulaya atapokea  kadi rasmi ya CHADEMA hapo alhamisi wiki hii.mtandao huu unaendelea kufwatilia nini hasa kitajitokeza katika hili

No comments: