Tuesday, July 14, 2015

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU,WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA AMANI NA UMOJA ULIOPO

Ikiwa imesalia miezi kadhaa kwa Tanzania  kuingia katika zoezi kubwa la uchaguzi mkuu,viongozi na wale wote wanaowania nafasi za uongozi wametakiwa kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unakuwa ni chanzo cha kukuza umoja na amani iliyopo Tanzania bila kusababisha aina yoyote ya vurugu ambazo zinaweza kuwagharimu watanzania.

Kauli hyiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na kiongozi mkuu wa mashia Tanzania sheikh HEMED JALALA katika muendelezo wa maadhimisho ya siku ya QUDS siku ambayo huazimishwa kila inapofika ijumaa ya mwisho kabla ya sikukuu ya IDD,siku ambayo waislam hao wameitumia kuhamasisha amani katika mataifa yanayokosa amani hiyo likiwemo taifa la palestina.


Akizungumza na wanahabari sheikh JALALA amesema kuwa amani katika taifa lolote ndio kiini cha maendeleo huku akisema kuwa viongozi wakubwa wa Africa kama mwalimu nyerere na nelson Mandela walifakiwa kukuza amani na kuisisitiza sana barani Africa hivyo ni jukumu la viongiozi wetu kuienzi amani iliyopo

Amesema kuwa siku ya QUDS ni siku ya kuwakumbuka wanyonge na wale wote ambao wanakumbana na dhuluma za aina mbalimbali hivyo wametumia siku hiyo kulikumbuka taifa la palestina likiwa ni taifa ambalo watu wake wamekuwa wakikumbana na adha hiyo ya kuonewa na kudhulumiwa ardhi yao taktribani miaka 67 sasa.

Ameongeza  kuwa waadhrika wakubwa katika nchi ambayo amani imekosekana kama palestina ni wazee,wakina mama,pamoja na watoto bila kujali dini zao wala kabila hivyo ni lazima dunia kwa umoja wetu tuamke na kuwatetea wananchi wa taifa la palestina ambao wanakumbana na mateso ya aina hiyo.


Amesema kuwa kiinachotokea nchini Palestina kinaweza kutokea katika taifa lolote hata Tanzania hivyo ni lazima kwa pamoja tuungane kuilinda na kuitetea amani tuliyonayo.

No comments: