Friday, July 24, 2015

KUTOKA MAHAKAMA KUU LEO,SHERIA YA KURA YA MAONI YAPINGWA

Mkurugenzi wa utetezi na maboresho wa kituo cha sheria na haki za Binadamu LHRC ambaye ndiye mwanasheria aliyesimamia ufunguaji wa shauri hili  HAROLD SUNGUSIA akizungumza na wanahabari mbalimbali waliofika mahakama kuu Jijini Dar es salaam.katikati ni ndugu RASHID SALUM ambaye ndiye mwananchi wa Tanzania aliyemua kufungua kesi hiyo ua kupinga sheria ya kura ya maoni namba 11 ya mwaka 2013
Kituo cha sheria na haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na mashirika mengine yanayotetea haki za raia leo wamefungua kesi ya kikatiba katika mahakama kuu ya Tanzania dhidi ya sheria ya kura ya maoni namba  11 ya mwaka 2013 sheria ambayo wamedai inavunja haki za msingi za Raia wa Tanzania ambao wapo katika kuamua hatma ya Taifa lao kupitia mchakato wa katiba mpya.EXAUD MTEI anasimulia zaidi---

Akizungumza mahakamani hapo na mtandao huu mara baada ya kufungua kesi hii mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za Binadamu LHRC HAROLD SUNGUSIA  amesema kuwa kituo hicho  kwa kushirikiana na mashirika mengine walipokea mteja ambaye alijimbulisha kama mwananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndugu RASHID SALUM  ambaye alitaka kufunguliwa kwa shauri la kikatiba katika mahakama kuu ya Tanzania kuiomba mahakama iweze kuamua juu ya ubatili wa baadhi ya vifungu vya sheria ya kura ya maoni namba 11 ya mwaka 2013 ambazo amesema zinakinzana na haki za msingi za raia katika katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Zoezi la ufunguaji wa shauri hilo ndani ya mahakama kuu nchini Tanzania likiendelea.hapa ni ndugu RASHID SALUM na mwanasheria KUTOKA lhrc HAROLD SUNGUSIA wakijadiliana jambo wakati wakifungua shauri hilo
Kwa mujibu wa mwanasheria huyo vifungu vinavyolalamikiwa ni pamoja na kifungu cha 34 (2),(b) ambacho kinatamka juu ya uhesabuji wa matokeo ya kura ya maoni kwa kujumuisha kura za wananchi wasio raia wa Zanzibar kuweza kupiga na kuhesabiwa kura zao kama wakazi wa Zanzibar ambapo amesema kifungu hicho kina lengo la kuwabagua watanzania ambao ni wakazi wa Zanzibar na kuwanyima haki ya kuamua kwa uhuru juu ya maswala yanayohusu muskabali wa taifa lao kwa kigezo cha uchache wao dhidi ya wingi wa raia wa Tanzania bara kinyume na ibara ya 13(2) inayokataza bunge kutunga sheria zenye ubaguzi dhidi ya raia na ibara ya 21(2) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977 inayompa haki mwananchi kuamua juu ya maswala ya taifa lake.
RASHID SALUM ambaye ni mwananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania aliyefungua shauri hilo leo akizungumza na wanahabari nje ya mahakama kuu Tanzania
Akizungumza na mtandao huu nje ya mahakama kuu jijini Dar es salaam mwananchi aliyewasilisha malalamiko yake katika shirika hilo ndugu RASHID SALUM amesema kuwa ameamua kufungua kesi hiyo ya kikatiba baada ya kugundua sheria hiyo ina madhara makubwa katika mchakato wa katiba mpya kutokana na kuwa sheria hiyo inampa mamlaka mwananchi wa Tanzania bara kumuwakilisha mkazi wa Zanzibar hata katika kufanya maamuzi juu ya mambo yanayohusu taifa lao.

Amesema kuwa kifungu cha 37 cha sheria ya kura ya maoni kinatoa mwanya mkubwa wa tume ya taifa ya uchaguzi ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kusimamia zoezi nzima la kura ya maoni kutumia vibaya madaraka hayo katika kuwezesha mazingira maalum ya upigaji kura ya maoni kwa makundi maalum kinyume na ibara ya 29(5) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

No comments: