Thursday, July 23, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONESHO YA 10 YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA VYUO VYA ELIMU YA JUU NCHINI.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kufungua  rasmi Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam.  Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo Julai 23, 2015. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mvumbuzi wa mashine ya kuchujia maji safi, Dkt. Askwar Hilonga, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo Julai 23, 2015. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha, Atilio Raphael (kushoto kwake) na William Sambera (kulia) kuhusu Kompyuta ya mezani waliyoibuni maalum kwa ajili ya kufundishia somo la Kompyuta, wakati Makamu alipotembelea Banda la Chuo hicho katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo Julai 23, 2015. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akioneshwa Plastiki zilizotengenezwa  kwa kutumia Mahindi kutoka kwa Mkurugenzi wa Chuo cha The United African University Of Tanzania (UAUT) Chang Kilee, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo hicho katika Maonesho ya 10 ya  Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo Julai 23, 2015. Picha na OMR



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja kati ya mashine za kufanya miamala za Max Malipo, huku akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko wa Kampuni hiyo, Machungu Msama,  wakati alipotembelea banda lao la maonesho katika Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo Julai 23, 2015. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tunguu Zanzibar, Hadi Mohamed  na baadhi ya wanafunzi wake, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo hicho kwenye Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya walimu, viongozi na wanafunzi wa Vyuo Vikuu. Picha na OMR





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo Julai 23, 2015. Picha na OMR

No comments: