Monday, July 13, 2015

NEC YATANUA GOLI ZAIDI,MAJIMBO MAPYA YA UCHAGUZI HAYA HAPA

Mwenyekiti wa Tume Jaji Damian Lubuva akitangaza Majimbo Mapya kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Julius Mallaba
Mwenyekiti wa Tume Jaji Damian Lubuva akitangaza Majimbo Mapya kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Julius Mallaba 
TUME ya Uchaguzi ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC)imetangaza Majimbo  26 mapya  ya Wabunge,,Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
      
Akiyatangaza Majimbo hayo leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema sababu iliyoifanya Tume hiyo kuongeza majimbo ya Uchaguzi imetokana na kuongeza kwa idadi ya watu,kuanzishwa  kwa wilaya mpya pamoja na Kuongezeka idadi ya nafasi viti ndani ya Ukumbi wa Bunge.
   
Jaji Lubuva ameyataja Majimbo hayo mapya  ambayo yametokana  na kuanzishwa kwa Halmashairi mpya ni jimbo la Mbinga Mijini,Jimbo la Madaba,Jimbo la Ndaba,Jimbo la Bunda Mjini,Jimbo la Newala,Jimbo la  Kondoa,Jimbo la Nzega Mjini,Jimbo la Usheti,
      
Mengine ni Jimbo la Ushetu,Jimbo la Kahama mjini,Jimbo la Mafinga,Jimbo la Geita,Jimbo la Kavuu,Jimbo la Nsimbo, Jimbo la Tunduma,Jimbo la Tarime,Jimbo la Butiama,
 Jimbo la Makambako,Jimbo la  Nanyamba pamoja na Jimbo la Handeni.

    Sanjari na hayo Jaji Lubuva ameyataja majimbo mengine  ambayo  yameongezeka kutokana na Idadi kubwa ya watu ni Jimbo la Mbagala – Dar es salaam ,Jimbo la kibamba – Dar es salaam,Jimbo la Vwawa – Mbeya ,Jimbo la  Manonga , Tabora Jimbo la Mlimba - Morogoro Ulyankulu - Tabora.

      Majimbo yaliyobadilishwa majina

1. Jimbo la Rungwe Mashariki Mkoa wa Mbeya, litaitwa Jimbo la Busekelo
2. Jimbo la Rungwe Magharibi Mkoa wa Mbeya, litaitwa Jimbo la Rungwe
3. Jimbo la Urambo Mashariki Mkoa wa Tabora, litaitwa Jimbo la Urambo.
4. Jimbo la Urambo Magharibi Mkoa wa Tabora, litaitwa Jimbo la Kaliua.
5. Jimbo la Njombe Magharibi Mkoa Njombe, litaitwa Jimbo la Wanging’ombe
6. Jimbo la Njombe Kusini Mkoa wa Mjombe, litaitwa Jimbo la Lupembe
7. Jimbo la Bariadi Mashariki Mkoa wa Simiyu, litaitwa Jimbo la Itilima.
8. Jimbo la Bariadi Magharibi Mkoa wa Simiyu, litaitwa Jimbo la Bariadi.
9. Jimbo la Kondoa Kaskazini Mkoa wa Dodoma, litaitwa Jimbo la Kondoa.
10. Jimbo la Kondoa Kusini Mkoa wa Dodoma, litaitwa Jimbo la Chemba.

No comments: