Thursday, July 16, 2015

PIGO-MADIWANI 10 WA CCM NA UDP WAJIUNGA CHADEMA,PICHA NA MAJINA YAO YAKO HAPA



Baadhi ya madiwani kama wanavyoonekana katika picha ambao wametoka katika vyama vya UDP na CCM katika wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wameamua kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


(Wa kwanza kulia) Ni diwani kata ya Sakwe Masunga Ngagani (UDP) akiongea na mamia ya wananchi waliohudulia katika uwanja wa michezo Dutwa wakati wa kutambulishwa kwao kujiunga na Chadema. (Kulia) ni Diwani wa kata ya Nyakabindi Benjamini Matondo.


Vyama viwili katika wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu CCM pamoja na UDP vimepata pigo kubwa baada ya madiwani wake wapatao 10 kutimkia katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa madai ya kuchoshwa na uongonzi wa vyama hivyo

Akiwataja majina madiwani hao Katibu Mwenezi Chadema wilayani Bariadi Martine Mogani, alisema kuwa kati ya hao, watatu ni kutoka CCM na saba kutoka UDP ambao ni Benjamini Matondo (UDP) Nyakabindi, Shiwa Danhi (UDP) Sapiwi na Gulya Nyembe (UDP) Ihusi.
Wengine ni Ruta Mahagija (CCM) Dutwa, Nhandi Madede (UDP) Ikungulipu, Matalu Mongobusia (UDP) Mwaubingi, Andrea Henoka (UDP) Nkindwabiye, Juma Nengelo (CCM) Somanda pamoja na Masunga Ngagani (UDP) kutoka kata ya Sakwe.



Mtia nia nafasi ya Ubunge katika jimbo la Bariadi Magharibi Seni Silanga kupitia Chadema, akiongea na mamia ya wananchi katika kata ya Dutwa wakati wa kutambulishwa kwa madiwani 10 waliojiunga na chama hicho.



Watia nia nafasi ya ubunge jimbo la Bariadi Magharibi kupitia Chadema.

Mgombea nafasi ya ubunge Godwin Simba kupitia Chadema akiongea na wananchi wa kata ya Dutwa.

No comments: