Tuesday, July 21, 2015

WANANCHI WAFANANISHA BVR NA FREMASON WAZIKIMBIA,TACCEO WAJA NA KASORO KATIKA UANDIKISHWAJI,WATAKA ZITATULIWE MARA MOJA

Mwenyekiti wa mtandao wa Asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi nchini Tanzania (TACCEO)Ms MARTINA KABISAMA (kushoto) akizungumza na wanahabari pembeni ni mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC ambao mcho waratibu wa mtandao huo Bi HELLEN KIJO BISIMBA.
Wakati zoezi la uandikishwaji wa daftari la kusumu la  mpiga kura kwa mfumo mpya wa BVR likitarajiwa kuingia Jijini Dar es salaam siku ya kesho baada ya kumaliza mikoani,tume ya taifa ya uchaguzi imetakiwa kuhakikisha kuwa kasoro zilizojitokeza katika zoezi hilo mikoani hazijirudii jijini Dar es salaam huku wakitakiwa kuhakikisha wanawarudia wale ambao hawakupata nafasi ya kujiandikisha ili waweze kupata haki hiyo.EXAUD MTEI anasimulia zaidi--------

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na mtandao wa Asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi nchini Tanzania (TACCEO) unaoratibiwa na kituo cha sheria na haki za binadamu  (LHRC) wakati wakitoa tathmini yao kuhusu mwenendo wa zoezi hilo lililokuwa linafanyika katika mikoa mbalimbali nchini.
Mjumbe wa kamayti ongozi ya TACCEO kutoka YOC PWANI bwana ISRAEL ILUNDE akizngumza na wanahabari katika mkutano huo kuhusu tathmini waliyoifanya katika zoezi hilo
Mwenyekiti wa mtandao huo Ms MARTINA KABISAMA akizungumza na wanahabari amesema kuwa kumekuwa na kasoro mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza wakati zoezi hilo likiendelea katika mikoa mbalimbali jambo ambalo amesema  limeathiri kwa kiasi kikubwa zoezi hilo kwa baadhi ya mikoa hivyo kuitaka tume kuchukua hatua za haraka ili kuhakikisha kuwa kasoro hizo hazijirudi.
Wanahabari wakichukua Taarifa hiyo
Moja kati ya mapungufu aliyoyataja ni pamoja na kukosekana kwa elimu ya mpiga kura kwa wananchi mbalimbali ambapo amesema kuwa wananchi wengi wamekuwa hawaelewi lengo kuu la kujiandikisha huku wengine wakiamini kuwa kama wanamiliki kadi za zamani za kupigia kura hawana haja ya kujiandikisha jambo ambalo limefanya wananchi wengi kuacha kujiandikisha kwa kukosa elimu madhubuti juu ya hilo.


Katika dhana hiyo ya kukosekana elimu ya mpiga kura Mwenyekiti huyo amesema kuwa kuna baadhi ya maeneo wanakijiji wameshindwa kujitokeza katika zoezi hilo wakilifananisha na zoezi hilo na maswala ya kichawi pamoja na FREMASON.

Ametolea mfano maeneo ya mafia ambapo wananchi waligomea zoezi hilo wakilihusisha na imani za Fremason,maeneo ya rufiji pale ambapo alama za vidole ziliposhindwa kutambuliwa na mashine za BVR baadhi ya watu walisambaza uzushi kwamba watu hao ni wachawi,huku kubwa zaidi ikiwa ni huko meru ambapo wananchi waligomea kujiandikisha wakiamini kuwa mashine hizo zinanyonya damu.

Kasoro nyingine zilizotajwa ni pamoja na vituo vya kujiandikisha  kuwekwa katika nyumba za ibada,hospitali na maeneo ya wazi,waandikishaji kutokuwa na elimu ya matumizi ya mashine za BVR,Baadhi ya vituo kutokuwa na mazingira rafiki kwa walemavu,wazee na wajawazito,kuharibika mara kwa mara kwa mashine za BVR kutokana na kufanya kazi kwa muda mrefu,ukosefu wa utaratibu maalum wa uandikishwaji,pamoja na kubadilika mara kwa mara kwa ratiba ya uandikishwaji jambo ambalo amesema pia limewafanya watu wengi kushindwa kujiandikisha.

Aidha kasoro nyingine ambazo zimetajwa kama kikwazo katika mchakato huo ni kukosekana kwa vifaa muhimu kwenye mashine za BVR,pamoja na tume kushindwa kabisa kuonyesha jitihada za dhati kwa wanafunzi wa vyuo,wagonjwa,na mahabusu walio magerezani ambao hadi sasa hawajaandikishwa na hakuna dalili za wao kupata haki hiyo ya msingi.

Ms KABISAMA amesema kuwa kutokana na kasoro hizo nyingi zilizojitokeza katika mchakato huo kuna idadi kubwa ya watanzania ilishindwa kujiandikisha hivyo kama tume hiyo ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha watanzania wanapata haki hiyo ni lazima wahakikisha kuwa wanawarudia wale ambao walishindwa kujiandikisha ili wapate haki hiyo.

Jiji la Dar es salaam linaingia katika siku yake ya kwanza kesho ya uandikishwaji wa dafrati la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR hii ikiwa ni baada ya zoezi hilo kupita katika mikoa mingine ya Dar es salaam.

No comments: