Monday, July 20, 2015

Wateja wa Tigo Pesa kuvuna faida ya bilioni 3.3 kwenye malipo ya kila robo mwaka

Kampuni ya Tigo Tanzania imetangaza malipo ya faida ya hisa za tigo pesa kwa wateja wake katika robo mwaka mwingine, malipo haya ni jumla ya kiasa cha pesa bilioni 3.314 sawa na dola za kimarekani milioni 1.8. Huu ni ugawaji wa faida ya robo ya pili kwa mwaka huu.

Lengo letu ni kuhakikisha kuwa wadau wote wa Tigo Pesa, ambao ni pamoja na wateja binafsi, mawakala wa reja reja na washirika wetu wa kibiashara ambao watashiriki kwenye gawio la faida hii ni kutokana na thamani ya kietronikia (e-value) ambayo wamehifadhi kwenye pochi zao za Tigo Pesa," alisema Mkuu wa Huduma za kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel.



Hii ni faida ya pili ya hisa kwa mwaka 2015 ambayo pia ni ya tano tangu Tigo ilipoanza kugawa faida inayotokana na akaunti za Tigo Pesa zinazoratibiwa na benki kubwa nchini Tanzania, kwa kweli tunafuraha kutangaza mgawanyo huu kwa watumiaji wetu waaminifu wa Tigo Pesa. Malipo haya yanaonyesha dhamira yetu ya kutoa huduma za kifedha kwa wateja wetu nchi nzima kwa ujumla, "alisema Swanepoel.



Tigo ni kampuni ya mawasiliano ya simu ya kwanza na pekee duniani hadi sasa kushirikisha faida zake zitokanazo na akaunti ya fedha ya simu za mkononi, katika mfumo wa ugawaji kwa kila robo mwaka, aliongeza.

Tunaamini ugawaji huu wa faida ya hisa ya Tigo Pesa katika mwaka 2015 utaleta unafuu kwa mamilioni ya watumiaji wa Tigo Pesa katika kufanikisha mipango yao ya kifedha. Mawakala wa Tigo Pesa wameona baadhi ya faida kubwa inayotokana na mpango huu kama wanavyoshuhudia ukuaji wa biashara zao. Haya ni matokeo ya kuongezeka kwa wateja na kushiriki faida, "alisema.
Swanepoel aliongeza kwa kusema kwamba, kabla ya faida kwa wateja huwa inakokotolewa kwa kuzingatia wastani wa salio la kila siku lililohifadhiwa kwenye pochi zao za Tigo Pesa. Malipo ya kiasi cha bilioni 3.314 yanakaribiana na yale ambayo kampuni ililipa katika robo mwaka ya kwanza ya mwaka 2015.




Mpango huu wa mgawanyo wa faida za hisa za Tigo Pesa ni kwa mujibu wa waraka wa Benki Kuu uliotolewa mwezi Februari 2014. Hadi sasa kampuni imelipa jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 27.2  kwa watumiaji wa Tigo Pesa katika robo tano za mwaka za malipo tangu kuanzishwa kwa huduma hii mwezi Julai 2014 .


No comments: