Monday, August 3, 2015

Story ya mnyika na Tundu lissu Kukihama chadema,Ubishi unaisha kwa picha hizi

Tangu chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA kibadilishe njia yake ya kuusaka uongozi wa Taifa hili kwa kumsajili waziri mkuu mstaafu Edward lowasa kumekuwa na story mfululizo zilizokuwa zinaeleza kuwa kuna baadhi ya viongozi wa chama hicho wamesusa kushiriki katika vikao vya chama hicho kutokana na kutokubaliana na uteuzi wa mh LOWASA.

Viongozi waliokuwa wanatajwa ni pamoja na mwasheria wa chama hicho Mh TUNDU LISSU,na Naibu katibu mkuu Bara mh JOHN MNYIKA ambao kwa pamoja walihusishwa katika sakata hilo.

Leo inaweza kuwa ni mwisho wa story hizo baada ya viongozi hao kuonekana katika mkutano mkuu wa baraza kuu la chama hicho KAMA PICHA ZINAVYOONYESHA  tofauti na wengi walivyodhani kuwa hawatashiriki katika vikao tena.

Mh  mnyika akizngumza na mwandishi wa mtanzao huu amesema kuwa sababu pekee iliyomfanya asionekane kwa kipindi kirefu tokea usajili wa LOWASA ufanyika ni matatizo ya kiafya na sasa yupo fiti kukitumikia chama hicho.


No comments: