.

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA TEMEKE (CCM) ABBAS MTEMVU AZINDUA KAMPENI ZAKE KWA KISHINDO DAR ES SALAAM

MGOMBEA ubunge jimbo la Temeke,kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) Abbas Mtemvu amekemea vikali viongozi wa chama hicho wanadharau wananchi baada ya kuchaguliwa kwakuwa wananchi ndiyo wenye mamlaka sahihi.Hayo yalisemwa na Mbunge huyo alipokuwa

akizindua rasmi kampeni yake ya jimbo hilo,ambayo ilihudhuriwa na wananchi zaidi ya 600 wenye mapenzi ya mgombea huyo,huku akisindikizwa na viongozi wa Chama hicho akiwemo Katibu Mwenezi wa Mkoa Juma Simba,Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Yahaya Sikunjema,na Madiwani wateule kama Noel Kipangule wa Chang'ombe,Francs Mtawa wa keko.

Alisema kuwa hawezi kunyama na kuvumilia mfumu wa baadhi ya viongozi kudharau wananchi wao baada ya kuchaguliwa  kwakuwa  wao sio wenye mamlaka ya kujichagua bali ni wananchi.

Alisema kuwa inasikitisha mno kuona wagombea wanakuja mikono nyuma kabla ya kupata lakini wanakuwa miungu watu baada ya kushinda.

Endelea kutizama picha zaidi zxa tuykio hiloAbout HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.