.

Simulizi nzima ya lowasa na UKAWA jana wakiwa Dar es salaam,Ahadi Kerm kem zatolewa

http://4.bp.blogspot.com/-6vYv_3XFd-c/VeuNBpnUuYI/AAAAAAAAkDk/rdpPdrHr-s8/s1600/2.jpg Na OPTATUCY STAN wa dar es salaamMgombea wa urais anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA BW EDWRD NGOYAI LOWASA  amewaahidi wakazi wa jiji la DAR ES SALAM kuwa kama atapewa ridhaa na wananchi ya kuwa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ataunda wizara maalum ambayo itakuwa inashighulikia changamoto za jiji la dare es salaam.
Akizungumza na mamia kwa maelfu ya wakazi wa eneo la chanika lililopo katika jimbo la ukonga llowasa amesema kuwa anatambua kero za jiji la dar es saalam ndomaana kama atapewa idhini na wananchi atahakikisha anamteuwa waziri ambaye akillala akiamuka kazi yake kubwa itakuwa ni kushughulika na kero ambazo zinawatesa wakazi wa jiji.


Lowasa ambaye aliwasiri eneo la chanika majira ya 8:26 mchana katika viwanja vya magenge alilakiwa na umati wa watu wengi tofauti na ilivyokuwa inadhaniwa awali.akizungumzia kuhusu propaganda zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa kam wananchi wakichagua upinzani nchi itaingia kwenye machafuko LOWASA iliwaomba wakazi wa eneo hilo kupuuza maneno hayo huku akisisitiza kuwa kama wananchi wataamua kumpa ridhaa atahakikisha anaunda selikali ambayo itakuwa rafiki kwa watu wa kada zote.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo  CHADEMA bw FREEMAN MBOWE aliwaomba wakazi wa eneo hilo kutoa ushirikiano kwa wananchi wengine ambao tayari wameshaamua kufanaya mabadiliko ili waweze kuwa sehemu ya wananchi wanaotaka kuingia kwenye selikali mpya inayojali haki na misingi ya utawala bora.

Sanjali na hayo mbowe alimtaka mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi jaji DAMIAN LUBUVA kukemea kwa vitendo kauli iliyotolewa na mjumbe wa kamati kuu ya chama cha mapinduzi bw Abdalla bulembo aliyoitoa mkoani kigoma kuwa chama cha mapinduzi kitaachi nafasi zote ila sio urais,Mbowe amesema kuwa tume ya taifa ya uchaguzi inapaswa kuzitolea maamuzi ya kiuhalisia kauli kama hizo kwani mwisho wa siku zinaweza zikasababisha machafuko.

Mgombea wa ubunge kupita ukawa jimbo la ukonga bw mwita waitara amesema jimbo la ukonga analijua sana hivo wana ukonga hawapaswi kufanya makosa tena kama ambayo wamekuwa wakiyafanya miaka mingine.waitara amesema kazi ni moja tu kwa wana ukonga kuhakikisha mara baada ya uchaguzi anatangazwa kama muwakilishi wao

LOWASA IKIWA ZAKIEM.Lowasa aliwasiri katika viwanja vya zakiem mbagar majira 11:30 huku akilakiwa tena kwa maelfu na maelfu ya wakazi wa kitongoji chenye wakazi wengi cha mbagara jijini  Dar es saalam,lowasa aliwambia wana mbagara kuwa kama wakimchagua atahakikisha kila mwananchi anatengenezewa mazingira bora ya  kuwa na maisha bora huku akiahidi kuwa elimu bora pamoja na kilimo cha kisasa vitawekwa mbele maana ndo sekta zinazowahusu watanzania wengi.

MBATIA AKIWA ZAKIEM. Mwenyekiti wa chama cha NCCR MAGEUZI BW JAMES MBATIA aliwambia wana mbagara kuwa ukawa wakiingia madarakani watafanya kazi ambayo watumwa na wananchi tofauti na wanachokifanya chama cha mapinduzi kwa sasa.Mbatia aliwasihi wakazi wa eneo hilo kuwa kiti limoja kwa sasa ili waweze kuleta mabadiliko ya kweli.BW mbatia ambaye pia ni mgombea wa ubunge kupitia umoja huo katika jimbo la vunjo aliwataka watu wote kuungana bla kujali tofauti zao na kufanya mabadilo yatakayowaletea neema ya maisha.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.