Thursday, September 24, 2015

VIDEO--MBATIA aikwarua Report ya TWAWEZA,Tizama alivyoichambua hapa

Na Exaud Mtei (Msaka Habari)
Umoja wa katiba ya wananchi Tanzania UKAWA leo umeitaka taasisi inayijihisisha na maswala ya midahalo na tafiti mbalimbali TWAWEZA kuandaa mdahalo wa wazi na umoja huo kwa ajili ya kuichambua na kuitetea tafiti yao waliyoitoa hivi majuzi inayoonyesha kuwa chama cha mapinduzi kina nafasi kubwa ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari kuhusu kile alichikiita kuwa ni utafiti wa kupikwa kwa maslahi ya watu mwenyekiti mwenza wa umoja huo JAMES MBATIA amesema kuwa TWAWEZA kama Taasisi inayojihusisha na uandaaji wa midahalo na kufadhili midahalo mbalimbali inayohusiana na uchaguzi mkuu wanawataka kuitisha mdahalo baina yao na viongozi wa umoja huo kwa ajili ya kuitetea taarifa yao hiyo.

Akizngumzia Taarifa hiyo ya TWAWEZA mh MBATIA amesema kuwa ni jambo jema kwa taasisi hiyo kushiriki katika maswala ya kukuza Democrasia ya Tanzania lakini wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa iliyotolewa na taaisis hiyo kutokana na kuonekana ina mapungufu mengi ya wazi ambayo hata mtu ambaye hajasoma anaona wazi kuwa ni utafiti wa kupikwa kwa ajili ya maslahi ya chama cha mapinduzi.huku akisema kuwa taaarifa hiyo inaonyesha wazi jinsi gani taasisi hiyo inatumika vibaya na chama cha mapinduzi kwa ajili ya kuwaahadaa wapiga kura na kawaaminisha kuwa chama cha mapinduzi bado kina uwezo wa kushinda.

Mh mbatia amesema kuwa pamoja na Taarifa zote lakini ni wazi kuwa taarifa hiyo imejaa propaganda,ambazo moja kwa moja zimelenga kukisaidia chama cha mapinduzi ambapo amesema kuwa jambo hilo limeidhalilisha sana taasisi hiyo.
Amesema kuwa kuna kasoro nyingi ambazo zipo katika utafiti huo na kufanya watanzania kupuuza utafiti huo huku akizitaja kadhaa kuwa ni –

1-Waliotafitiwa walipewa simu za bure na watoa utafiti,ambapo katika taarifa hiyo imeandikwa kuwa simu za mkononi pamoja na chaja,zinazotumia chaji mwanga wa jua ziligawiwa kwa kaya shiriki.

2-Watafiti wenyewe wanaonekana kudhani kuwa UKAWA ni chama ambapo katika ukarasa wa kwanza wa taarifa hiyo mgombea anayewakilisha ukawa ni EDWARD LOWASA.

3-Kutothamini kwa usawa,michango,ya vyama vinavyoshiriki uchaguzi huu mkuu,vyama kama ADC,CHAUMA,NLD,NRA,na UPDP havikuwekewa takwimu za moja kwa moja ambapo vilihesabika kama vyama vingine.

4-Kuorodhesha vyama visivyokuwa na wagombea Urais katika swali la kuchagua Rais kwa mfano CUF,NCCR-MAGEUZI.
5-Maana ya UKAWA ni “Walinzi wa katiba ya wananchi”ndivyo utafiti unavyoeleza katika uk 11 aya ya kwanza.

6-Jumla ya asilimia kwa wima kutokuwa 100,katika kila jedwali kwenye ukurasa wa 8,9 na 10 kwa mfano kwenye jedwali ukurasa wa 8,jumla nya asilimia chini ya mwaka 2013 ni 82badala ya 100,kwenye jedwali la ukurasa 9,ujumla cjhini ya mwaka 2015 ni 102,kwenye jedwali la ukurasa wa 10 jumla chini ya mwaka 2014 ni 85

7-Mtafiti hawezi kutafiti kitu anachokijua ambapo katika ukurasa wa 10 imeandikwa ikumbukwe kuwa UKAWA imejumuishwa katika kielelezo hiki ili kuonyesha kuwa wananchi wanadhani kwamba UKAWA ni chama ,UKAWA haijasajiliwa kama chama cha siasa

8-Majumuisha ya Matokeo ya utafiti hayaendani na maswali ya utafiti kwa mfano katika ukurasa wa 7 swali ni Je uchaguzi ungefanyika leo ungempigia kura mgombea wa chama gani,wakati jumuisho la tafiti huo linasema kuwa CCM ndio chama nkinachopendwa zaidi na wanaowaunga mkono CHADEMA wamepungua kidogo tangu mwaka 2013.

9-Kauli nyingi zinakinzana mfano\
(A)          Katika ukurasa wa 12 imeandikwa kuwa utafitri huu sio utabiri lakini katika majumuisho katika ukurasa wa 15 imeandikwa kuwa “karibu wananchi wote 99% wanasema kuwa watapiga kura katika”
“Zaidi ya 60% walisema kuwa wantamchaguz mgombea wa CCM wa Urais,ubunge na udiwani”
“26% ya wananchi watamchagua kwa sababu hii..

B)          Katika Ukurasa wa 12 swali lilikuwa “ukimwacha Rais Kikwete iwapo uchaguzi wa rais ungefanyika leo ungemchagua nani?”
“Chanzo cha takwimu wahojiwa hawakupatiwa orodha ya kuchagua
  

Mh MBATIA amesema kuwa kutokana na maswala hayo yaliyojitokeza ni wazi kuwa utafiti huo hauna nia njema kwa uchaguzi wa mwaka huu,huku akiwaomba watanzania pamoja na wapenda maendeleo na mabadiliko kutoitilia maanani Taarifa hiyo na kuwataka watanzania waendelee kuilinda na kuitunza amani kwani tafiti kama hizo za kupikwa zinaweza kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani kwa watanzania.

No comments: