WLAC waendelea kuwajengea Uwezo wadau kuelekea uchaguzi mkuu,leo zamu ya wanavyuo

Wanafunzi mbalimbali kutoka vyuo Tofauti  nchini Tanzania wakiendelea kushiriki katika mafunzo hayo maalum yaliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la kituo cha msaada wa kisheria kwa wanawake WLAC mafunzo ambayo yamefanyika Jijini Dar es salaam
 Shirika lisilo la kiserikali la linalotoa msaada wa kisheria kwa wanawake nchini  WLAC kwa kudhaminiwa na OXFARM leo wameendelea na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa makundi ya watu mbalimbali nchini kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi mkuu na jinsi gani makundi hayo yanaweza kuutumia uchaguzi huo kupata viongozi wanaowataka.
Baada ya wiki iliyopita shirika hilo kuwakutanisha wakina mama mbalimbali ambao walikuwa viongozi wa VICOBA wilaya ya kinondoni hatimaye leo shirika hilo limewakutanisha wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini ambao kwa pamoja wamepata na kubadilishana mawazo jinsi ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Bi FORTUNATA MAKAFU akiendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa wanafunzi wa vyuo  waliojitokeza katika mafunzo hayo Leo Jijini Dar es salaam
Akizungumza na wanahabari wakati wa mafunzo hayo leo mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo Bi FORTUNATA MAKAFU amesema kuwa pamoja na ushiriki wa vijana katika uchaguzi huu kuonekana ni mkubwa lakini bado changamoto kubwa ipo kwa vijana hao kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ambapo amesema hilo bado ni changamoto kwani vijana wengi wamehamasika katika uchaguzi lakini bado hawajahamasika kuwania nafasi kama za udiwani na ubunge.
Washiriki wakisikiliza kwa Makini
Amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuendelea kuwajengea uwezo vijana hao na kuwapa hamasa ya kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi wa mwaka huu ili waweze kuwachaguzi viongozi ambao watawasaidia katika kuwakwamua na hali iliyopo sasa.
Mmoja kati ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Tanzania aliyejitambulisha kama AMOURE ELISHADAI akizungumza na wanahabari juu ya mafunzo hayo ambayo amesema kuwa yamemsaidia sana katika kuelekea uchaguzi wake ambapo sasa amepata mwanga juu ya kushiriki kikamilifu katika hatua zote za uchaguzi wa mwaka huu ili kama kijana aweze kupata kiongozi ambaye atamsaidia katika kumletea maendeleo
Aidha amesema kuwa moja ya mambo ambayo wanajaribu kuwaelekeza vijana kwa sasa ni kuwa wachambuzi wa mambo hasa kipindi hiki cha kampeni kwa kusikiliza na kuchambua ni kiongozi yupi ana uwezo wa kuwasaidia kwa dhati na kuepuka muhemko ya kisiasa ambayo inaweza kuwapatia vijana viongozi ambao hawana nia dhabiti kwa watanzania.
Mshiriki DYNA STEVEN ambaye naye amekiri kupata msaada mkubwa wa kimawazo na kifikra katika mafunzo hayo ya leo

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.