Friday, October 23, 2015

KAULI YA TACCEO LEO KUHUSU YANAYOENDELEA KWENYE UCHAGUZI KWA SASA

Mwenyekiti wa mtandao wa asasi za kiraia unaoangalia chaguzi nchini Tanzania Bi MARTINA KABISAMA akizungumza na wahabari mapema leo Jijini Dar es salaam
 Mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi nchini Tanzania TACCEO unaoratibiwa na kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC umepinga vikali hatua ya maelekezo ya nyongeza yaliyotolewa na tume ya taifa ya uchaguzi huku wakisema kuwa ni hatua ambayo inaweza kuvuruga uchaguzi wa Tanzania.

Akizungumza na wanahabari mapema leo mwenyekiti wa mtandao huo unaojumuisha asasi za Kiraia zaidi ya 17 mama MARTINA KABISAMA amesema kuwa TACCEO imepokea kwa masikitiko makubwa na mashaka hatua ya tume kutoa maelekezo hayo ambayo yalitoka kama maelekezo ya ziada katika uchaguzi.

“Sisi tunatambua na kuheshimu haki ya wananchi kupiga kura katika chaguzi za kidemocrasia,pia tunatambua kuwa wapo baadhi ya wananchi ambao kwa namna moja au nyingine hawataweza kupiga kura kwa sababu mbalimbali ikiwemo baadhi yao kukosa majina yao katika daftari la mpiga kura,pamoja na matatizo mengine kama hayo,pamoja na umuhimu huo tunasikitishwa na tume ya taifa ya uchaguzi kutoa maelekezo ambayo huenda yakafungua mwanya na watu wasiostahili kupiga kura au kuruhusu baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu kutumia mwanya huo kupiga kura zaidi ya mara moja”amesema mwenyekiti huyo wa TACCEO.

Maelekezo ya tume hiyo yalilenga kuruhusu watu ambao vitambulisho vyao havitakuwa na picha au vitakuwa na picha iliyofutika kuruhusiwa kupiga kura,huku pia tume ikiruhusu wapiga kura ambao wana kadi ya mpiga kura lakini majina yao hayako kwenye daftari waweze kupiga kura hatua ambayo imeanza kutiliwa mashaka na wadau mbalimbali na kuamua kupinga swala hilo.

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC ambao ni waratibu wa TACCEO Bi HELLEN KIJO BISIMBA akizungumza
Aidha Mtandao huo leo wametoa tathmini yao ya kampeni za uchaguzi mkuu tathimini ambayo imeonyesha kampeni hizo kukumbwa na changamoto na maswala mbalimbali ambayo wametaka kufanyiwa kazi ili uchaguzi huu uweze kuwa wa huru na haki.

Akizungumza na wanahabari mapema leo mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za bunadamu nchini Bi HELEN KIJO BISIMBA amesema kuwa lengo kuu la kufwatilia na kuangalia mwenendo mzima wa uchaguzi huo ni kujiridhisha kwa kiwango ambacho Tanzania inatekeleza kwa vitendo majukumu yake ya kikatiba na sheria mbalimbali zinazoongoza uchaguzi huo.
Moja kati ya viongozi wanaoongoza zoezi hilo la uangalizi HAMIS MKINDI
Katika tathmini ambayo imefanywa na waangalizi ambao wapo kila kona ya nchi kutoka TACCEO wamebaini mambo kumi makubwa ambayo yalikiukwa kwa kiasi kikubwa katika kampeni huku wakitaka maswala hayo yasijirudie katika kipindi cha upigaji kura kwani yanaweza kuharibu sura ya uchaguzi mkuu.

Akiyataja mambo hayo Bi HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa swla la muda katika kampeni lilikuwa chagamoto ambapo jumla ya mikutano 172 ilimalizika juu ya muda uliopangwa na tume ya uchaguzi jambo ambalo lilijitokeza kwa vyama vyote nchini,Matumizi ya lugha za kudhalilisha utu nalo limetajwa kama kikwazo na tatizo kubwa ambalo lilijitokeza katika kampeni hizo,ambapo mikutano 188 iliyohudhuriwa na waangalizi wa TACCEO ilikuwa imegubikwa na matusi na lugha za kudhalilisha utu wa mwanadamu.
Wanahabari wakichukua Taarifa hiyo
Maswala mengine ambayo wameyataja kwenye Tathmini yao ni kuzuiwa kwa kampeni na vyombo vya dola,kampeni za vitisho na kauli za chuki,Matumizi ya rasilimali za umma,matumizi mabaya ya vyombo vya habari,wananchi kugawiwa pesa au vyakula,kufanyika kwa kampeni katika majengo ya ibada,pamoja na uharibifu wa mabango,bendera na vifaa vya kampeni vya vyama,ni maswala ambayo yamejitokeza kwa wingi.

No comments: