UKAWA WAJIPA USHINDI WA 61%,NI UTAFITI WAO WA MWISHO KUFANYIKA

Mkurugenzi wa Uchaguzi Wa CHADEMA Bwana REGNALD MUNISI akizungumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam
Na Exaud Msaka Habari
Chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA kwa kupitia umoja wa katiba UKAWA wametangaza kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na vyama hivyo nchi nzima wamejihakikishia ushindi wa asilimia 61% katika uchaguyzi mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani unaotaraji kufanyika jumapili ya wiki hii nchini Tanzania.

Akizungumza na wanahabari mapoema leo mkurugenzi wa uchaguzi wa chama hicho Bwana REGINALD MUNISI ametanabaisha kuwa kila chama cha siasa kina utaratibu wake wa kuangalia ni jinsi gani kinakubalika na ushindi aina gani kinaweza kupata katika ucgauzi ambapo amesema wao wamekuwa wakitumia mfumo wa kawaida wa Pool ambazo ni Tafiti wanazofanya mikoa yote Tanzania ili kupioma wana nafasi gani katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Amesema kuwa kuwa mujibu wa Utafiti waliofanya mwishoni mwa wiki jana(wikiend iliyopita) na kuwahusisha watanzania zaidi ya elfu 30,Umeonyesha kuwa umoja wa katiba ya wananchi kupitia mgombea wao wa Urais Edward Lowasa ana nafasi ya kushinda kiti hicho kwa asilimia 61% ya kura zote ambazo zitapigwa nchini Tanzania.huku akisema kuwa wana imani ndani ya siku zilizobaki hakiwezi kubadilika kitu kikubwa katika takwimu hizo.

Bwana Munisi amesema kuwa chama hicho pamoja na umoja wa katiba ya wananchi sasa umejiridhisha wazi kuwa wanakwenda kushinda kwa kishindo katika uchaguzi wa mwaka huu hivyo wapenzi na watanzania kutokuwa na hofu ya aina yoyote kuhusu amani ya Tanzania.

Katika hatua nyingine vyama hivyo vimeitaka serikali iliyoppo madarakani kuwapa wananchi wa Tanzania kuamua hatma ya nchi yao kupitia sanduku la kura na kupitia katiba ya Tanzania kwani kumeanza kuonekana aina ya vitisho ambavyo amesema kwa namna moja ama nyingine vinaweza kuwafanya watanzania kuwa na hofu juu ya uchaguzi huo.

Amesema kuwa ni wazi kumekuwa na vihoja vingi,na maneno mengi ambayo yamekuwa yakisemwa na wapinzani wao yakiwa na lengo la kuwaaminisha watu kuwa wapinzani hawana uwezo wa kushinda ambapo amesema kuwa kupindi kama hiki ni lazima maswala hayo yajitokeza ambapo amesema sio kikwazo katika ushindi wa uchaguzi wa mwaka huu.


Aidha umoja huo wametangaza rasmi kuwa kampeni za mgombea Urais wa chama hicho Edward Lowasa zitafungwa siku ya tarehe 24 katika viwanja vya jangwani Jijini Dar es salaam ambapo mipango ya shughuli hiyo inaendelea na itakapokamilika itawekwa wazi

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.