Video--Breaking newzz--UKAWA watua umoja wa mataifa na ICC uholanzi,ni sakata la Rais KIKWETE..SOMA HII

Hatimaye chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA Pamoja na umoja wa katiba ya wananchi UKAWA wameandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Ba Ki-moon,Barua ambayo pia imeenda katika mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ya ICC,pamoja na jumuiya za kimataifa,barua  imnayowasilisha malalamiko ya vyama hivyo juu ya kile walichoita kauli za vitisho na rafu zinazifanywa na serikali juu ya vyama hivyo kuelekea uchaguzi mkuu wa wiki ijayo.

Akizumgumza na wanahabari mapema leo mwanasheria wa chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA JOHN MALLYA amesema kuwa wameamua kuandika barua hiyo kutokana na kile walichoita ni kauli za vitisho zilivyotolewa na Rais wa Tanzania JAKAYA KIKWETE juu ya wananchi jambo ambalo amesema wametaka kutoa taarifa katika taasisi hizo na kuhoji kama ni sahihi kwa Rais kutoa kauli kama hizo.

Amesema kuwa maamuzi ya kuandika barua kwa taasisi hizo yamekuja kutokana na uwazi kuwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania huwezi kumshataki Rais kutokana na kinga aliyonayo hivyo wameona ni muhimu kufikisha swala hilo kwa jumuiya za kimataifa ili waendelee kuitambua hali halisi inayoendelea na kama wanaweza kutoa maelekezo kwa Rais kuacha kuwatisha wananchi kipindi hiki cha uchaguzi.

Kauli ambazo zinalalamikiwa na Umoja huo ni kauli aliyoitoa Rais Kikwete juu ya swala la wananchi kukaa meter mia mbili kulinda kura ambapo aliagiza vyombo vya dola kuwashiughulikia wote ambao watafanya hivyo huku vyama hivyo vya upinzani wakisisitiza kuwa swala hilo lipo kisheria na kuendelea kuwahamasisha wananchi na wanachama wao kulinda kura baada ya kumaliza kupiga kura zao.


Barua hiyo iliyopelekwa asubuhi ya leo  ambayo imesainiwa na makamu mweyekiti wa CHADEMA Profesa ABDALA SAFARI imepekekwa pia nakala zake common wealth London,African Union,pamoja na mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ya uholanzi ICC.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.