Wednesday, October 21, 2015

Wananchi wa Kibada wajichanga wenyewe kupata kupata Gari la zima moto

Mwenyeikiti wa kamati ya maandali iliyofanikisha upatikanaji wa Gari hilo la zima moto Bwana MUSA BIBOSE Akitoa maelekezo kwa wananchi waliohudhuria shughuli ya uzinduzi wa gari hilo Kigamboni Kibada Jijini Dar es salaam 


Mwenyekiti wa Umoja wa wananchi wa Kibada Kigamboni Jijini Dar es salaam Bwana LUGANO MWAMPETU akizungumza katika Hafla ya makabidhiano ya gari moja ya zimamoto iliyofanyiwa marekebisho na wananchji wa kibada kwa Juhudi za umoja huo na kuzinduliwa leo na Kamishna wa Operation Jeshi La Zima moto na uokoaji Tanzania CP ROGATUS P-KIPALI LEO Kigamboni.


Kamishna wa Operation Jeshi La Zima moto na uokoaji Tanzania CP ROGATUS P-KIPALI akiangumza na wananchi waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa Gari hilo ambapo amewapongeza wananchi wa Kibada kwa juhudi kubwa za kuhakikisha kuwa wanaleta maendeleo katika maeneo yao.


Mwenyeikiti wa umoja wa wananchi wa KIBADA kigamboni Jijini Dar es salaam LUGANO MWAMPETU akimpa maelekezo kamishna wa Operation jeshi la zima moto na uaokoaji Tanzania CP ROGATUS P.KIPALI wakati wa shughuli ya kumkabisdhi gari moja la zima moto lililofanyiwa marekebisho kwa nguvu ya wananchi wa kibada kwa ajili ya kuwasaidia wakazi hao na majanga ya moto,shughuli iliyofanyika kigamboni Kibada Jijini Dar es salaam Tarehe 20,10,2015.

Gari ambalo limefifuliwa na umoja wa wananchi wa Kibada kwa ajili ya kuwasaidia wakazi wa kigamboni na majanga ya moto
Askakari wa zima moto wakifanya majaribio ya kuonyesha ufanyaji kazi wa gari hili

No comments: