Monday, November 23, 2015

ALPHONCE MAWAZO--Hajazikwa Hadi sasa hiki ndicho kinachoendelea

Baada ya zoezi la kuuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo kushindikana kutokana na jeshi la polisi mkoani Mwanza kupiga marufuku mikusanyiko ya wanachama na wafuasi wa chama hicho kwa madai ya kuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu jijini Mwanza, hatimaye viongozi wakuu wa kitaifa wa Chadema pamoja na familia ya marehemu wameamua kwenda mahakamani kutafuta haki yao ya kisheria.Mwenyekiti wa Chadema taifa Mh. Freeman Mbowe anajitokeza mbele ya waandishi wa habari na wabunge 45 wa kambi ya upinzani kutoa msimamo wa chama hicho baada ya vikao vya mashauriano. Waziri mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye pamoja na aliyekuwa mgombea urais kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) Mh. Edward Lowassa nao wametoa angalizo kwa jeshi la polisi nchini.
Mchungaji Charles Lugiko ni baba wa marehemu Alphone Mawazo anakielezeaje kitendo cha askari polisi kwenda hadi nyumbani kwake eneo la Nyegezi na kuwatawanya waombolezaji? 
Makamu mwenyekiti wa Chadema Zanzibar Issa Said Mohammed ni kati ya viongozi wakuu wa kitaifa wa chama hicho waliokwenda katika kijiji cha Chikobe ambako marehemu atazikwa, je ni nini alichokiona huko?
  
Alphonce Mawazo aliuawa kikatili kwa kukatwa mapanga na mashoka na watu wasiojulikana Novemba 14 mwaka huu katika kijiji cha katoro wilayani Geita.

Edward Lowassa alaani vikali kitendo cha Serikali kuwanyanyasa waie wote waliokuwa wakiunga mkono upinzani. 





No comments: