Monday, November 9, 2015

HALI ZANZIBAR YAENDELEA KUWA TETE,WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI CUF WAIBUKA DAR,WAPINGA KUFUTWA KWA UCHAGUZI

Naibu katibu mkuu wa Chama Cha wananchi CUF, Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na waandishi wa habari leo katika mkutano wa waandishi wa habari leo kuhusiana na wabunge wa baraza la wawakilishi Zanzibar kumwomba rais wa jamhuri ya muungano kuwaapisha ili waanze kufanya kazi yao kwaajili ya kuwawakilisha wananchi wa majimbo yao.
Mgombea wa baraza la wawakilishi Zanzibar, Abubakari Khamis akionyesha fomu ya  uthibitisho kuwa amechaguliwa kuwa mwakilishi wa baraza la wawakilishi Zanzibar leo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
STORY NA PICHA KWA MSAADA WA MICHUZI BLOG(

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wa Chama chama Wananchi (CUF)wamepinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kufutwa  kutokana na mtu aliyefanya utenguzi huo ni utashi wake na sio Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Wajumbe 27 wa baraza hilo wamewasili jijini Dar es Salaam kuzungumza na waandishi wa habari juu ya kizungumkuti cha matokeo ya uchaguzi kufutwa huku wakiwa wenyewe hatambui hatua hiyo.

Akizungumza  mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Abbakari Khamisi amesema uchaguzi wao uliofutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha hawatambui na wataka waendelee kuhesabu kura hizo na sio kurudia uchaguzi.

Amesema uchaguzi utafutwaje wakati wajumbe wa baraza la wawakilishi wamepata udhibitisho wa maandishi wa kushinda majimbo yao na kufanya uchaguzi ukirudiwa ni ukiukwaji kwa katiba.

Khamisi amesema kuwa uchaguzi wa Zanzibar, kushinda kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ni halali na kushinda chama kingine kati uchaguzi unaonekana batili huku wakujua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

“Hatutaki uchaguzi urudiwe kwani kufanya hivyo ni kukiuka kwa katiba ya uchaguzi kutokana  na waangalizi walisema uchaguzi ulikuwa wa haki na huru kwa nini urudiwe wakati katiba haina tafsiri ya kufuta na matokeo na kufanya uchaguzi mwingine”amesema Khamisi.

Nae Ismail  Jussa mshindi wa jimbo la Marindi amesema kuwa hawatambui kuendelea kwa utawala uliopo sasa kutokana na katiba ya Zanzibar.


 Aliongeza kuwa nchi ya Zanzibara haina Rais na kufanya kuendelea kwa Rais aliyemaliza muda wake ni kukiuka kwa katiba.

Baadhi ya wajumbe wa bunge la wawakilishi Zanzibar wakionyesha fomu zao za Ushindi wa walipohudhulia mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

No comments: