Mwenyekiti wa Jukwaa la katiba nchini Tanzania JUKATA akizungumza na wanahabari kuhusu maswala kadhaa kuhusu katiba mpya Tanzania ambapo wamemshauri Rais wa Tanzania DR MAGUFULI kuhakikisha kuwa mchakato wa katiba mpya unaanza upya ili uweze kutoa nafasi ya ya kupata nafasi ya kupata katiba iliyotokana na maoni ya wananchi. Na Exaud Msaka Habari |
Jukwaa la katiba Tanzania
JUKATA wamemtaka Rais mpya wa Tanzania Mh DR JOHN POMBE MAGUFULI kuhakikisha kuwa kasi yake na kauli mbiu yake
ya HAPA KAZI TU ianzie katika mchakato wa kupata katiba mpya ambapo wamemtaka
kuhakikisha kuwa anaanza upya mchakato wa kupata katiba mpya na kupata katiba
ambayo imepatikana kutokana na maoni wananchi wa Tanzania.
Akizungumza na
wanahabri mapema leo jijini Dar es salaam mwenyekiti wa Jukwaa la katiba nchini
Tanzania JUKATA DEUC KIBAMBA amesema kuwa ili Rais mpya aweze kukamilisha adhma
yeka na ya watanzania wengi ya kuleta
mabadiliko na mageuzi katika mfumo wa kiuongozi wa Tanzania ni lazima
ahakikishe kuwa mchakato wa katiba mpya ambayo ndiyo pekee inayoweza
kubadilisha mfumo wa Tanzania.
Amesema kuwa mpango
alioanza nao Mh MAGUFULI wa kufanya ziara za kushtukiza pekee haitoshi kuleta
mabadiliko ya kiutendaji nchini Tanzania bali mabadiliko ya kweli yatatokana na
utendaji uliobadilika wa mfumo mzima wa serikali ambao utaletwa na katiba inayojali
maoni ya wananchi.
Bwana DEUS KIBAMBA
amesema JUKATA wanamtaka Rais wa Tanzanaia DR MAGUFULI baada ya kuzindua bunge
na kupata mawaziri wake ahakikishe kuwa kwanza analitangazia Taifa Rasmi namna ya
kurejea mchakato wa kupata katiba mpya,serikali ipeleke bungeni miswada ya
mabadiliko ya serikali zinazosimamia mchakato wa katiba,kurejea makubaliano ya Dodoma
ambayo yalitaka pia kupanua wigo wa wadau wahusika katika mchakato wa kupata
katiba ikiwemo pia nyama vya wafanyakazi,ambapo amesema kuwa kama rais atafanya
hayo anaweza kushinda mtihani wa serikali yake kuaminika na watanzania walio wengi.
Katika hatua nyingine
jukwaa la katiba nchini Tanzania JUKATA wamemtaka Rais wa Tanzania DR MAGUFULI
aweze kuongoza jitihada za kuinusuru Zanzibar kutumbukia kwenye mkwamo au
machafuko ya kisiasa hali ya sintofahamu iliyojitokeza baada ya uchaguzi ikiwa
ni pamoja na kutambua kuwa hatua ya umoja wa serikali ya kitaifa iliyokuwa
imeshafikiwa na wanzanzibar inapaswa kulindwa na kuheshimiwa.
Bwana KIBAMBA amesema
kuwa kwa mujibu wa waangalizi wa JUKATA waliokuwa wakiangalia uchaguzi wa Zanzibar
wameonyesha kuwa uchaguzi huo wa zanzibar ulifanyika na kumalizika kwa amani na
hakukuwa na dosari kubwa zilizokuwa zinaweza kuwafanya uchaguzi huo kuahirishwa
hivyo wameshangazwa sana hatua ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar Kufuta
uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment