Wednesday, November 25, 2015

TIGO YADHAMINI ONESHO LA MWANAMUZIKI MOUSSA DIALLO KUTOKA NCHINI MALI LITANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM KESHO

Meneja wa Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo, John Wanyanja (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kampuni hiyo kudhamini onesho la mwanamuziki Mousa Diallo kutoka nchini Mali litakalofanyika kesho katika Mgahawa wa Chakula na Vinywaji wa Samaki Samaki, Masaki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Masoko wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Saum Wengert na katikati ni Mwanamuziki, Moussa Diallo.
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo, John Wanyanja (kushoto), akizungumza na Mwanamuziki, Moussa Diallo (kulia). Katikati ni Mmiliki wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Carlos Bastos.
Mwanamuziki Moussa Diallo wa nchini Mali anayeishi Denmark (katikati), akiimba mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akijitambulisha ambapo leo atafanya onesho lake Ukumbi wa Samaki Samaki, Masaki jijini Dar es Slaam. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo, John Wanyanja ambao wamewezesha ujio wa mwanamuziki huyo na kushoto ni Ofisa  Mkuu wa Masoko wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Saum Wengert.
Ofisa Mkuu wa Masoko wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Saum Wengert (kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu onesho hilo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Warembo wa Samaki Samaki wakifuatilia matukio mbalimbali ya mkutano huo.
…………………………………………………………………………………………..Na Dotto Mwaibale
MWANAMUZIKI maarufu toka Afrika Magharibi anayeishi Denmark, Moussa Diallo, leo anatarajia kufanya onesho lake hilo leo (Novemba 26) katika Mgahawa wa Chakula na Vinywaji wa  Samaki Samaki uliopopo Masaki jijijini Dar es Salaam ambapo litaenda sanjari na ziara ya kutembelea  miradi mbalimbali ya kijamii hapa nchini.


Onesho hilo lililodhaminiwa na Kampuni  ya simu za mikononi ya Tigo ikishirikiana na Mgahawa huo wa  Samaki Samaki litafanywa na Mwanamuziki huyo toka nchini Mali mwenye asili ya Denmark, ambaye amewasili nchini leo.


 Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi kwenye mkutano wa waandishi wa habari, Ofisa Mkuu wa Masoko wa Samaki Samaki, Saum Wengert, alisema mwanamuziki huyo anapiga muziki wa aina ya soul iliyochanganywa na vionjo vya kiafrika na muziki wa Magharibi unaopendwa ulimwenguni kote.


 Alisema onesho hilo pia linatarajiwa kufanyika kesho kutwa (Novemba 27) katika Hoteli ya Melia jijini Zanzibar na baadae watafanya Full Moon Party kwenye Hotel ya Kendwa Rocks iliyopo jijini Zanzibar. 


Moussa alizaliwa jijini Paris nchini Ufaransa na kukulia Bamako nchini Mali ambapo hivi sasa anamakazi yake Copenhagen nchini Denmark.


Katika juhudi za kukuza utamaduni, Diallo anachanganya muziki wake kwa kushirikisha vikundi mbalimbali vya utamaduni ikiwemo; Dawda Jobarten (Kora, Mwimbaji), Preben Carlsen (gitaa), Salieu Dibba (Percussions, Sauti), na Marco Diallo (Ngoma).


Kwa upande wake, Meneja uhusiano wa Tigo, John Wanyacha alisema kampuni hiyo na wadhamini wengine wamekubali Diallo kufanya onesho nchini ikiwa ni pamoja na kuweka mahusiano mazuri yaliyopo na maonesho yanayokuja.


Alisema kuwa wanafahamu wanachopenda wateja wao kwenye muziki na kwamba wana eneo ambalo linaweza kuwawezesha kuzuia miziki wasioyoipenda hivyo ujio wa Diallo nchini utaendeleza makubaliano mazuri kati ya kampuni hizo kwa kuwapa wateja wanachokihitaji ikiwa ni pamoja na vionjo. 

Wengine waliodhamini ziara hiyo ni pamoja ni; Johnnie Walker, French Kiss, Heineken na Ledger Plaza Bahari Beach.


(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments: