Selikali imeaswa kushughulikia kesi za uchaguzi kwa wakati ili
kuepusha wananchi kukosa haki yao ya msingi ya uwakilishi bungeni kwa wakati
huo ambao watakuwa hawana uwakilishi ndani ya chombo hicho cha wananchi.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mwenyekiti wa (TACCEO) BW ISRAEL ILUNDE
wakati alipokuwa akitoa Ripoti ya awali ya uchaguzi wa mwaka huu uliofanyika octaber 25
mwaka huu.report ambayo imekluja huku kukiwa bado kuna sintiofahamu ya vifaa
kadhaa vya waangalizi hao vikiwa bado vimeshikiliwa na jeshi la polisi kwa kile
kilichoitwa kukiuka sheria mbalimbali za uangalizi wa uchaguzi wa ndani.
Mmoja wa Waratibu wa mtandao huo HAMIS MKINDI akifafanua jambo katika Mkutano huo |
Bwana Ilunde ameeleza kuwa uangalizi wao
umebaini kutotekeleza majukumu kwa wakati kulikokuwa kunafanywa na tume ya Taifa
ya uchaguzi akitolea mfano kitendo cha kuchelewesha vifaa vya kupigia kura
katika maeneo mbalimbali na baadhi ya maeneo kushindwa kufanya uchaguzi
kutokana na kukosekana kwa vifaa kwa wakati jambo ambalo wamesema kuwa
lilitokea katika maeneo kadhaa hapa nchini.
Aidha Ilunde alisema kwa miaka mingi kunakuwaga na ucheleweshaji
wa kesi za uchaguzi jambo linalopelekeaga wananchi wa eneo husika kukosa
uwakilishi na hatimaye jimbo lao kutofanya maendeleo
Kaimu Mkurugenzi wa LHRC ambao ndio waratibu wa TACCEO akizungumza katika mkutano huo |
Kwa upande wake Mratibu wa mtandao huo Bw HAMIS MKINDI amesema
kuwa tume ya taifa ya uchaguzi lazima iwe inachukulia changamoto zinazojitokeza
kwenye uchaguzi husika kama somo kwa uchaguzi mwingne kwani zipi changamoto
nyingi ambazo zilijitokeza.
Sambamba na hilo BW MKINDI amevishauri vyombo vya dola kusimamia
haki ili Taifa liweze kuongozwa kwa misingi ya uwazi,haki na uadilifu
Wanahabari wakipata habari |
Aidha wakizungumzia kizungumkuti kilichochojitokeza visiwani
zanzibar, waangalizi hao wametangaza kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na haki
lakini wanashangazwa na tume ya uchaguzi ZEC kushindwa kumtanga mshindi mpaka
sasa.
Kaimu mkutugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC
ambao ndio waratibu wa mtandao huo wa TACCEO Bi EMELDA LULU URIO alisema
waangalizi wao wote walionyesha kuwa uchaguzi wa Zanzibar haukuwa na dosari
yoyote hivyo ni matarajio yao ZEC itamtangza mshindi na siyo zoezi la kurudia
kupiga kura.
No comments:
Post a Comment