Friday, November 13, 2015

WASAMBAZAJI WA FILAMU ZA NJE WATAKIWA KUFUATA SHERIA YA UKAGUZI WA FILAMU.

WS1
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akisisitiza jambo juu ya Sheria ya Ukaguzi wa Filamu nchini kwa baadhi ya wawakilishi wa Wasambazaji wa Filamu za nje nchini wakati walipokutana ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam.Picha na Frank Shija, WHVUM
WS2
PIX2: Mmoja wa wasambazaji wa filamu za nje nchini Bw. Joseph Lyakurini (wa kwanza kushoto) akielezea jambo wakati wa kikao baina ya Wasambazaji wa Filamu za nje na Bodi ya Filamu nchini kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.
WS3
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akizungumza na baadhi ya wawakilishi wa Wasambazaji wa Filamu za nje nchini wakati walipokutana ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Na: Frank Shija, WHVUM
Wasambazaji wa Filamu za nje wametakiwa kuwasilisha filamu wanazosambaza katika ofisi za Bodi ya Filamu kwa ajili ya ukaguzi mapema ifikapo tarehe 30 mezi huu.
Agizo hilo limetolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo wakatio wa kikao chake na Wasambazaji hao jana jijini Dar es Salaam.
Fissoo amesema kuwa kwa agizo hilo linatokana na matakwa ya kisheria ambapo kila filamu kabla ya kufikishwa kwa walaji ni lazima ikaguliwe na kupangiwa madaraja na Bodi ya Filamu nchini.
“Ninatoa wito kwamba ifikapo Novemba 30 maka huu wasambazaji wote wa Filamu za nje wawe wamewasilisha kazi zao katika ofisi yangu kwa ajili ya ukaguzi”Alisema Fissoo.
Aidha Fissoo amesema kuwa kwa ameamua kutoa agizo hilo kutokana na kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria ya Ukaguzi wa Filamu nchini hasa kwa filamu za nje.
Kwa uande wake mwakilishi wa wasambaji wa Filamu za nje Bw. Joseph Lyakurini ameiomba Bodi ya filamu kuwasaidia katika kuwajengea mazingira rafiki ya utekelezaji wa agizo hilo kwa kushirikisha taasisi zote zinazohusika katika biashara ya Filamu nchini.
Bw. Joseph ameongeza kuwa wao binafsi wakotayari kutekeleza agizo hilo japo chanagamoto kubwa wanayokumbana nayo ni suala la hatimiliki suala ambalo linawakatisha tamaa.
“Mheshimiwa Katibu tukuombe tu utusaidie kupata wepesi katika kutekeleza agizo lako hasa suala zima la hatimiliki ya filamu zinazotoka nje.” Alisema Joseph.
Ukaguzi wa Filamu nchini upo kwa mujibu wa sheria ya ukaguzi wa filamu no.4 ya mwaka 1976 ambapo filamu yeyote inapaswa kukaguliwa na kupangiwa daraja kabla ya kusambazwa au kuonyeshwa hadharani.

No comments: