Friday, December 11, 2015

LUDOVICK UTOUH ATWAA TUZO KUTOKA LHRC,TIZAMA ALICHOSEMA KUHUSU SERIKALI YA MAGUFULI

Mgeni Rasmi katika hafla hiyo Mchungaji STEVE MUNGA akimkabidhi Tuzo ya majimaji aliyewahi kuwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali LODOVICK UTOUH Tuzo ambayo inatolea na Kituo cha sheria na haki za Binadamu kila mwaka kwa Mtumishi aliyejipambanua katika kupambana na haki za binadamu na utawala bora nchini katika kipindi cha utumishi wake,UTOUH anakuwa Mtanzania wa Tatu kunyakua Tuzo hiyo.
 Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa miaka nane katika awamu iliyopita Ludovick Utouh ameibuka na kuipongeza kasi aliyoanza nayo Rais wa awamu ya tano Mh JOHN MAGUFULI huku akisema kuwa kasi hiyo inahitaji msaada kutoka kwa watendaji wa chini kwani Rais hana uwezo wa kushughulikia kila wizara bila msaada wa watendaji wenye moyo wa kazi.
Kaimu Mkurugenzi wa LHRC Wakili EMELDA LULU URIO akizungumza katika hafla hiyo
Mh Ludovick Utouh katika hafla ya kumkabidhi tuzo kiongozi huyo iliyotolewa na Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini LHRC tuzo inayoitwa Tuzo ya maji maji,tuzo ambayo inatolewa kila mwaka kwa mtu au kiongozi ambaye katika utendaji wake amejipambanua kulinda haki za binadamu pamoja na kutetea utawala bora,tuzo ambayo kwa mwaka huu ni mara ya tatu kutolewa na kwenda kwa mdhibiti huyo na mkaguzi wa hesabu za serikali mstaafu Ludovick Utouh
Mchapalo ukiendelea
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Tuzo hiyo Utouh alisema kuwa ni furaha kuona kazi aliyoifanya inatambuliwa na watu na mashirika mbalimbali na kuamua kumpongeza jambo ambalo amesema kuwa ni furaha kwake na kuona kuwa kazi aliyoifanya ni msada kwa watanzania waliowengi.
Alisema kuwa wakati wa utendaji wake aliamua kusimamia ukweli na haki hasa katika maswala ya ufisadi na matumizi mabaya ya Mali za watanzania ambapo wakati mwingine alionekana kama hana nia njema na serikali yake lakini hiyo ndiyo iliyompa heshima katika nafasi hiyo.

Wafanyakazi wa Kituo cha sheria na Haki za Binadamu nchini Wakiongozwa na Kaimu mwenyekiti wa kituo hicho EMELDA LULU URIO wakiwa wamebeba Tuzo hiyo ambayo ilinyakuliwa na LUDOVICK UTOUH.
Akizungumzia uamuzi wa Rais MAGUFULI wa kuwaondoa wabunge wote katika bodi za mashirika ya UMMA amesema kuwa hilo ni jambo lililokuwa linamshangaza sana katika seikali ya awamu ya Tano kwani ilikuwa haileti maana mbunge ambaye anatakiwa kuihoji serikali na kuisimamia anakuwa ni mmoja kati ya wanaonufaika na serikali hiyo jambo ambalo liliwafanya wabunge wengi kushindwa kuhoji maswala nyeti ya serikali kwa kulinda maslahi yao.
Mazungumzo ni sehemu ya Furaha 
“Nilikuwa kila siku nadai hili swala la wabunge kuwepo katika Bodi za mashirika ya UMMA,hadi nilionekana kama mtu mbaya sana,ila nilichokuwa nasimamia niliakiamini,nashukuru sana kwa Rais Mpya kuamua kufanya hivyo kwani itawafanya wabunge sasa kuwa huru kuihoji serikali katika maswala nyeti na makubwa”Alisema Ludovick Utouh
Alitolea mfano sakata la ukwapuaji wa fedha za ESCROW lilivyokuwa linajadiliwa bungeni akasema kuwa kuna baadhi ya wabunge walikuwa hata hawaelewi waongee nini,wengine ukiwasikia hujui hata wanaongea nini,wengine walikaa kimya yote kwa sababu swala hilo na wao wapo katika mashirika hayo,ila sasa naamini kuwa serikali nitakwenda.

Tuzo ya Maji Maji hutolewa kila mwaka na kituo cha sheria na haki za Binadamu Lhrc ambapo kwa tuzo ya kwanza ilikwenda kwa Mr. Justice (Rtd.) Mwalusanya,na ya Pili ilikwenda kwa Katibu mkuu wa zamani wa CHADEMA ambaye alikuwa Mbunge DR WIBROD SLAA baada ya kuonekana kupambana na ufisadi akiwa bungeni ambapo ya tatu imekwenda kwa Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali msataafu Ludovick Utouh

No comments: